Watoto wawili majeruhi wa ajali ya gari la Shule ya Lucky Vincent wameruhusiwa kutoka hopitalini.
Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ameandika katika ukurasa
wake wa Facebook kuwa watoto hao, Sadia Ismael na Wilson Tarimo
waliokuwa wamelazwa katika hospitali ya Mercy ya Marekani wameruhusiwa
na sasa wapo katika makazi mapya.
“Watoto Sadia na Wilson waruhusiwa rasmi kutoka hospitali ya Mercy na
wanaelekea kwenye makazi yao mapya mjini Sioux City IA. Mungu azidi
kuwaangazia nuru ya uso wake. Amani iwe nawe na Nesi wetu mpendwa kwa
huduma kubwa mmefanya kwa watoto hawa na Tanzania,”ameandika Nyalandu.
Jana Nyalandu aliandika kuwa mtoto Doreen ataendelea kuwepo hospitali
katika wodi ya watoto akiendelea kupata huduma za karibu hadi
itakapoamuliwa vinginevyo.
Post a Comment