PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: BAADA ya Waandishi wa Habari Kukamatwa na Kuachiwa na Polisi Jana Mkoani Arusha..Nape Nnauye Ametoa Lake la Moyoni..!!!
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Mbunge wa Jimbo la Mtama Mh. Nape Nnauye ameshauri vyombo vya usalama nchini vitimize majukumu yao pasipo kutumia nguvu s...



Mbunge wa Jimbo la Mtama Mh. Nape Nnauye ameshauri vyombo vya usalama nchini vitimize majukumu yao pasipo kutumia nguvu sehemu ambayo mazungumzo yanaweza kuwa na tija ili kuendelea kulinda nchi katika namna nzuri ya kushirikiana. 

Mh. Nape amesema kuwa vyombo vya dola vimekuwa ni vyombo vya wananchi

"Ni vizuri vyombo vya dola vikatimiza wajibu wao na ni vizuri tukalinda nchi yetu katika mazingira ambayo tumekuwa tukihusiana kwa muda mrefu, vyombo hivi vya dola hivi vimekuwa ni vyombo vya wananchi na ndio maana jeshi letu linaitwa jeshi la Wananchi wa Tanzania, si vizuri kutumia nguvu kubwa pale ambapo hapahitajiki kutumia nguvu kubwa. Na mimi nimeendelea kushauri nchi yetu bado tumeendelea kufanya mambo yetu kwa mazungumzo kwa kuelewana" alisema Nape Nnauye 

Mbali na hilo Nape Nnauye anasema mambo haya ya polisi kutumia nguvu sehemu isipohitajika nguvu yanajenga chuki kati ya wananchi na serikali yao. 

"Nchi yetu hatukuzoea hayo, nchi yetu hatukuzoea mabavu, kwanza matendo haya yanajenga chuki kati ya serikali na wananchi, yatajenga chuki kati ya Rais na wananchi, yatajenga chuki kati ya CCM na wananchi kwa sababu itafika mahali wananchi hawakuzoea mambo haya watajenga chuki tu kuona nchi yetu haiendi sawasawa" alisisitiza Nape Nnauye

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top