PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: TUNAWAENZI VIPI WANAMICHEZO WETU ???
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
         Na. Lonana Lameck ole Kip PMT    17 Julai 2015 ilikuwa ni siku ya majonzi kwa ulimwengu wa michezo hasa hasa kwa upande wa mch...
   
 Image result
   Na. Lonana Lameck ole Kip PMT   

17 Julai 2015 ilikuwa ni siku ya majonzi kwa ulimwengu wa michezo hasa hasa kwa upande wa mchezo wa mashindano ya magari yaendayo kwa kasi mnoo ya Formula 1 almaarufu Langalanga , ilikuwa ni siku ambayo nyota ya kijana aliyekuwa akiija kwa kwa kasi kweny michuano hiyo kuzimika ghafla angalii akiwa bado ni kijana mdogo wa miaka 23 tuu , huyo si mwingine bali ni Hayati Jules Bianchi aliyekuwa akiitumikia timu ya Marussia na akiipeperusha vyema bendera ya Taifa la Ufaransa kwenye michuano hiyo mikubwa kabisa ya mbio za magari duniani . Lakini hivi majuzi tuu serikali ya Ufaransa kushirikiana na Mamlaka ya jiji la Nice alipozaliwa Jules Bianchi waliamua kuipatia Barabara inayounganisha mitaa kadha maarufu ya Jiji hilo jina lake na hivyo kuijulikana kama Jules Bianchi Road , kama heshima ya mchango wa Jules kwenye kuitangaza taifa lake hilo kwa ulimwengu wa Formula 1 ambapo aliipata ajali mwaka 2014 baada ya hitilafuu kutokeakwenye gari lake aina ya Ferrari kabla ya kuwa mahututi na kupoteza maisha mwaka uliofuata wa 2015 .                                           

 Lakini hiyo ikiwa haitoshi huko kunako visiwa vya Madeira nchini Ureno aliipozaliwa Gwiji la soka nchi humo Christiano Ronaldo ambaye anaitumikia klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania , Ronaldo ambaye ndiyo mfungaji bora wa muda wote kweny kikosi cha Ureno , alkuwa anapokea heshima kubwa kutoka kwa uongozi wa serikali wa mji anatokea wa Madeira kuamua kubalisha jina la uwanja wa ndege kutoka kuitwa Madeira Airport mpaka kuitwa Christiano Ronaldo Airport ni raha ilioje pale unapo litumikia taifa lako kwa juhudi kubwa na unakuja kulipwa zaidi ya kile ulichokipigania . 

Kama hiyo haitoshi katika jiji la Port of Spain nchini Trinidad & Tobbago huko nako kuna zawadi kubwa mnoo aliyopewa mchezaji mpira tuu , hakuwa kiongozi wa kiserikali kama tulivyozoea sisi ambao ndiyo hutunukiwa heshima kubwa kwa kupewa majina ya Madaraja , mitaa , majengo , barabara , viwanja vya mpira na kadhalika , bali yeye alikuwa kaptein wa taifa lake tuu akiliwakilisha katika michuano mbali mbali huku akionyesha utii na nidhamu ya kutosha anapokuwa akiwaongoza wenzake kupigania taifa lao , mpaka kufikia kupewa heshima ya uwanja wa taifa kupewa jina lake ambalo ni The Dwight Yorke National Stadium , kwa wasiomfahamu Dwight Yorke ndiyo Mtrinidad wakwanza kutwa kombe la klabu Ulaya akiwa na Manchester United masimu 1998/99 huku akitoa mchango mkubwa kwa klabu hiyo ikiwa ni pamoja na kutwa makombe Matatu makubwa kwa msimu ' Major Trophies ' kwenye msimu wa 1998/99 . Yorke alianza kupata umaarufu wake akiwa na klabu ya Aston Villa akifunga magoal maridhawa , akipiga chenga murua lakini pia akionyesha ushirikiano mkubwa na wachezaji wenzie jambo lilomshawishi Kocha wa Man United Mzee Sir Alex Ferguson kumnunua . 

Lakini nje ya klabu Yorke aliparangana kama sio kupigania taifa lake mpaka likafuzu kwa mara ya kwanza kwenye michuano mikubwa ambayo kila mchezaji ana ndoto ya kuyacheza , mwaka 2006 Trinidad & Tobbago waliiwakilisha ukanda wa CONCAF nchi zinazopatikana kwenye visiwa vya Carribean katika Kombe la Dunia nchini Ujerumani , japo waliishia hatua ya makundi tuu lakini ilitosha kuonyesha uwepo wao katika michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya timu ya Taifa . Kwa upande wetu Tanzania kuenziwa kwa wanamichezo limekuwa ni jambo lisilokuwa na mantiki yeyote japokuwa Mkoani Pwani kuna Shule shule ya Filbert Bayi shujaa aliyeweza kuitolea jasho Tanzania katika michuano kadha wa kadha ya kukimbiza upepo na kunyakua medali katika Olimpiki , michuano ya jumuiya ya Madola ' Common Wealth ' , All African Games na mingine kadha wa kadha . Lakini bado naona wavuja jasho walioipigania Taifa hili kwenye nyanja ya michezo bado hawathaminiwi ipasavyo , mfano John Akwarre mmoja kati ya mashuja kwenye Olimpiki ya 1968 Mexico City nchini Mexico hakushinda kitu chochote kwenye michuano hiyo lakini alionyesha 

Uzalendo mkubwa kwa Taifa lake ikiwa ni baada ya kuumizwa vibaya na viatu alivyokuwa amevivaa alipokuwa akikimbia Full Marathon kilometa 42 na kumpelekea kushindwa kukimbia vizuri na kumfanya kuwa washiriki wanaburuza mkia kwenye mbio hizo hali hiyo hamkufanya kushindwa kumaliza mbio hizo japo alikuwa na maumivu ya jeraha , Akwarre alimaliza mbio hizo akiwa wa mwisho lakini alipohojiwa kuhusiana na kwanin aliamua kumaliza mbio hizo wakati hashinda kitu chochote !?? , Mbulu huyo aliwajibu alikwenda kuwakilisha Taifa langu hivyo kumaliza mbio hizi lilikuwa ni suala la lazima kwangu . Pamoja na uzalendo wote huo wa John Akwarre lakini hata hata mtaa unaoitwa kwa jina lake nchi Nzima iwe Dar es Salaam au Mbulu anapoishi shujaa huyu na hata makazi yake bado ni duni . 

Mashujaa wetu sio wanasiasa tuu wapo hata kina Peter Tino shujaa aliyeweza kupachika magoli maridhawa na kuihakikishia Tanzania tiketi ya kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 1980 nchini Nigeria , ikiwa ni mara ya kwanza na mwisho mpaka leo hatujawahi kushiriki Afcon , wapi ilipo shule ya Petr Tino Primary School au hata Peter Tino Road sjawahi hata kuskia Peter Tino Street kitu tunachoskia ni nyumbani kwa Peter Tino pekee wakati nae alivuja jasho kwa taifa hili kwa Uzalendo huku akipokea posho kiduchu lakini aliwakilisha taifa lake mpaka tone la mwisho la jasho lake .

 Tuna mashujaa wengi na kituu ambacho nashindwa kuelewa ni kwanin hatuwapi heshima yao wanayostahili wakati wao walituheshimu mnoo kwa kutuwakilisha kwenye michezo kadha wa kadha , inafikia siku akijaakututoka anakuondoka na historia yake ambayo kumbukumbu yake inakuwa hafifu mnoo mpaka uitafute na tochi . 

Jijini Florence nchini Italia kuna sanamu kubwa tuu lililopo nje ya Uwanja wa Fiorentina klabu kongwe nchini Italia na Ulaya kwa ujumla ,  sanamu hilo ni la Gabriel Batistuta ' BatiGoal ' mshambuliaji aliyeichezea klabu hiyo kwa mafanikio makubwa japo ni mzaliwa wa Buenos Aires nchini Argentina lakini Waitaliano hawakujalii wakaamua kutengeneza sanamu la Striker huyo wa Kiargentina kama kuweka ukumbusho kwa vizazi vijavyo vimfahamu Batistuta alikuwaje , kama Waitaliano hawajalii wao wanaonyesha heshima tuu bila kuangalia Utaifa inakuadje sisi Watanzania tunashindwa kudhamini michango ya wanamichezo wetu .

 Natamani kuona au kuskia Rashid Matumla road au Suleiman Nyambui Bridge , Kibadeni Street na majina mengine yalivuja jasho kwa maslahi ya taifa . Tutakuwa tukilalamika kila siku kuhusiana kushuka kwa kiwango kwa Wanamichezo nchini lakini sisi wenywe ndiyo wasababishi sababu tunashindwa kuwaenzi wanamichezo wetu , tuamkeni na tuanze kuwaenzi wanamichezo wetu ili kuamsha ari miongoni mwa vizazi vijavyo vinavyochipuki .                        

  Mwandishi wa makala haya ni Mwanafunzi katika chuo cha Uandishi wa Habari Arusha A.J.T.C ngazi ya diploma
 Mawasiliano +255 653 835048                                      
  Email . lonanalameck3@gmail.com

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top