PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: TUNAMUENZI VIPI HAYATI SHEIKH ABEID KARUME !!
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
          Na Lonana ole Kip PMT             Ikiwa imetimia miaka 45 tangu kuzimika ghafla kwa taa iliyokuwaa ikiangaza Tanzania , Taa ...
        
 Na Lonana ole Kip PMT            

Ikiwa imetimia miaka 45 tangu kuzimika ghafla kwa taa iliyokuwaa ikiangaza Tanzania , Taa hiyo ilikuwa ikimulikaa gizani na kutoa mwangaza kwa watu wote walikuwa wakipita gizani kupata nuru ya kuwaonyesha njia salama , wasikanyage matope , maji , miba wala kitu chochote cha madhara dhidi yao . 

Baada ya kuanguka kwa taa hiyo mambo mengi yalipata kwenda mrama , Taa ninayoizungumzia ni Hayati Mzee Amir Abeid Karume moja kati ya wanasiasa na viongozi shupavu wa kizazi chake , ambapo tarehe 7 Aprili 1972 alipigwa risasi na fedhuli iliyokatisha maisha yake kama taa iliyozimika ghafla bin vuu . 
Babu yetu huyu ambaye alikuwa kiongozi hodari mnoo akisifika kwa kuchapa kazi muda wote huku akitekeleza ahadi zake zikiwamo kutoa elimu bure , makazi bora kwa wananchi wa Zanzibar na kadhalika . 

Kwa wakati huo ndiyo kwanza Zanzibar imefanya mapinduzi ya kuuondoa utawala wa Kisultan uliokuwa ukitawala kisiwa hicho kwa zaidi ya Karne 1 lakin pia ikiwa ni miaka kadha tangu kuunganika na Tanganyika na kuunda Tanzania . 

Babu yetu Mzee Karume alikuwa mstari wa mbele kujenga umoja na ushirikiano miongoni mwa wananchi , huku akipinga ukoloni mambo leo , uwepo wa aina yeyote ya kukandamizwa kupitia mabwanyenye , wakoloni na hata wafanyabiashara waliokuwa wakiwakandamiza wajiriwa wao . Ama kwa hakika Mzee Karume alikuwa mwamba miongoni mwa miamba , na yamkini hilo linajidhirisha miongoni mwetu kumuona Babu yetu Karume akiwa amewekwa kwenye Pesa yetu lakini pia jina lake kutumika kama heshima kwenye Viwanja vya michezo na vya usafiri . 

Pamoja na hayo lakini kwa Wanamichezo tunamuenzi vp Nahodha huyu ambaye nae alikuwa mwanamichezo hodari hasahasa wa mchezo wa Bao na michezo mingine ya asili , uwepo wa Uwanja wa kumbukumbu wa Sheikh Amri Abeid Karume jijini Arusha hautoshi kuenzi mchango wa Mzee wetu huyu ambaye aliweza kuleta mabadiliko makubwa kwenye nyanjaa zote , Mnamo mwaka 1971 mwaka mmoja kabla ya kifo chake alitoa wazo kwa klabu zetu kuacha kutumia majina ya kimgharibi na kutumia majina ya kwetu , wazo lake au kauli yake hiyo ilipokelewa vyema na viongozi wa klabu hizo ambazo kwa wakati huo klabu zilizokuwa zikivuma zilikuwa ni Sunderland Sports Club ambao walibadilii jina kujiita Simba Sports Club mpaka wa leo wamebakii na hilohilo jina huku wengine walikuwa ni Dar es Salaam Young Afrikans ambao walijibatiza jina la Yanga Afrika Sports Club mpaka wa leo hii , kwa hali hiyo haishangazi kumuona Bibi Fatma Karume akiwa ni mmoja wa wadhamini wa klabu ya Yanga Afrikans kutokana na upenzi mkubwa wa michezo aliokuwa nao Mzee ndiyo ukamfanya hata Bibi Fatma ajikite kwenye bodi ya wadhamini wa klabu hiyo kongwe nchini . 

Mzee wetu huyu pia alihubiri umoja na mshikamo miongoni mwa Wananchi huku akitilia mkazo kwenye Uzalendo kwanza , suala ambalo halitiliwi mkazo na wananchi na hata wadau wa michezo hii inatokana na kushindwa kuchangia timu zetu kabla ya michuano lakini baada ya kupata matokeo mabovu tunaanza kuwalaumu kama wamecheza chini ya kiwango huku tukijisahau kuwa tulishindwa kuonyesha Uzalendo kwa kuwachangia walipokuwa wakihitaji mchango wetu .

 Ama kwa hakika ni mengi mno tunashindwa kuzingatia kutoka kwa Babu yetu huyu ambaye leo hii ni maadhimisho ya kifo chake akiitimiza miaka 45 tangu atangulie mbele za haki , mida umefika kurudisha uzalendo uliokuwa umepotea , huku tukitilia mkazo yale yote tuliyoaswaa na Babu yetu Sheikh Amir Abeid Karume . Innalillahi Wainalillah Rajoun , Wote tumetoka Mavumbini na ndipo Tutakapo Rejea Amin .
  
Mwandishi wa makala haya ni Mwanafunzi katika Chuo cha Uandishi wa Habari Na Utangazaji Arusha A.J.T.C    Kwa maoni na Ushauri usisite kuwasiliana nami kupitia Namba +255 653 835048 .

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top