NA: ANDREA A. NGOBOLE PMT
Kila binadamu mwenye akili timamu hupenda kufanikiwa ili
kuwa na maisha mazuri yenye kupata hitaji lake la moyo na yampendezayo kila mara ila ni binadamu wachache sana wanaotafuta
mafanikio ya kweli na kufanikiwa kimaisha na hapo ndio linapotokea gape kubwa
kati ya walio nacho na wasiokuwa nacho nina maana hapo ndiyo tofauti iliyopo
kati ya maskini na tajiri.
Mtu asiyetafuta mafanikio ni mtu mwenye sifa zifuatzo kwanza
ni mvivu wa fikra hapendi kuishughulisha akili yake katika kutafuta mafanikio
huishia kuwa na malalamiko na kuona changamoto ndani ya jamii yake badala ya
kuona fursa katika changamoto inayoikabli jamii, hupenda kujadili watu na
maisha yao badala ya kujadili namna gani ya kuweza kufanikiwa kiuchumi, hupenda
kutumia Zaidi ya akipatacho katika pesa zake, hupenda kukopa na kushindwa
kulipa deni na hivyo kujiongezea maadui badala ya marafiki, huona aibu kufanya
kazi anayodhani inamzalilisha na mwisho wa siku huishia kuugulia maumivu ya
jeraha la moyo kwa kukosa pesa na kutafuta visingizio visivyo na kichwa wala
miguu mfano serikali imebana pesa au ajira ngumu kupata wakati anamiliki simu
ya gharama kubwa.
Watu wasiofikiria mafanikio hufikiria Zaidi katika njia za
mkato na kudhani njia hizo za mkato zitamletea mafanikio maishani, mfano
mwanafunzi asiyejiandaa na masomo yake vizuri ategemee aje anunue mtihani
afaulu masomo yake huenda akafanikiwa ila ni kwa muda mfupi sana kwani uwezo
utakuwa mdogo katika utendaji wake wa kazi.
Mfano mfanyabiashara asiyelipia kodi biashara yake kwa
kutaka short cut ya kufanikiwa siku akigundulika huenda biashara yake ikafa
kabisa kwani atafilisiwa na mamlaka husika za utozaji wa kodi na ndio hao ambao
hufikiria Zaidi kuhonga ili kupitisha mzigo siku njia zikibanwa ndio hao
utasikia anafunga biashara na kutoa visingizio kwa serikali iliyopo madarakani.
Asiyefikiria mafanikio vema hawezi kufuata utaratibu
uliowekwa wa kutenda kazi zake vizuri
bali huishia kufanya kwa mazoea na hivyo kuonekana hana umuhimu wowote na ndio
huwa wa kwanza kufikiria kutumbuliwa na wenye mamlaka ya kumtumbua.
Ni sawa na mtu ambaye wiki nzima hajafanya kazi yoyote ya
kumuingizia kipato lakini huyo huyo anafikiria weekend kutoka na kwenda kula starehe katika kumbi za
starehe na burudani za muziki wa dansi au wa kizazi kipya ina maana anapenda
starehe lakini hapendi kufanya kazi huyu mafanikio atayasikia kwenye bomba tu hawezi kufanikiwa kwani mafanikio
hayampendi mtu asiyeyatafuta.
Mtu anayetafuta mafanikio ana muda mchache sana wa kulala
kwani yeye hufikiria Zaidi ni jinsi gani atajikwamua kiuchumi kwa kubuni miradi
midogomidogo itakayomuingizia kipato cha uhakika, hujadiliana mambo ya msingi
ya kufanya ili aweze kujiongezea kipato chake halali, hawaamini katika njia ya
mkato ili kufanikiwa, hujituma kila siku za maisha yao kuhakikisha wanapata
kile kinachwaongezea kipato chao cha kila siku.
Mfano kilimo hakihitaji njia ya mkato lazima uandae shamba,
ulime kwa trekta au plau, upande mbegu uweke mbolea na umawagilie maji mbegu
ili ziote na zikishaota lazima upalilie na usubiri kwa muda flani ndio upate
mazao husika na kuvuna mazao yako na mafanikio pia yanahitaji uvumilivu huo
kama wa mkulima mwenye busara ya kujituma ipasavyo na kuamini atapata mazao ya
kile alichopanda.
Ili ufanikiwe inakulazimu kwanza kujitengenezea jina la
biashara yako mwenyewe yaani wewe mwenyewe uwe biashara kama una kipaji cha
kuimba imba sana itengeneze sauti yako iwe bora nay a kuvutia, kama ni kucheza
mpira cheza sana na ufanye mazoezi mpaka uwe tegemeo kwa timu yako na wengine
wakuone pia, kama kudansi fanya mazoezi ya kutosha kukuza kipaji chako ili
kikulipe kwani kila mmoja wetu ana kipawa chake chenye uwezo tofauti na mwezake
ndiyo maana tuna wanamuziki wengi lakini wenye vipaji vyao wamedumu mpaka leo tunasikiliza
nyimbo zao kama wakina Marijani Rajabu na wachezaji mpira bora kabisa kama Pele
na wengineo.
Mtu anayetafuta mafanikio huwekeza katika kutafuta maarifa
kila siku yatakayomfanikisha kujua namna ya kujikwamua kiuchumi yaani husoma
sana vitabu vyenye maarifa ya ujasiriamali, haogopi kuuliza maswali ya msingi
yatakayompa majibu sahihi kwa biashara ama kazi yake toka kwa watu anaoamini
kuwa wana maarifa sahihi, huambatana na watu wanaofanana kifikra ili
kujiongezea fikra chanya za mafanikio yake na hupenda sana kujiridhisha kabala
ya kuwekeza katika biasharea flani pia wote wanazungumza lugha moja ya biashara
wanamaneno yenye mvuto masikioni mwa wateja hawaongei lugha za mtaani.
Huwatambua wateja wake na hata wakiongezeka huwa hawaridhiki
nao hutafuta wateja wapya kila siku na hujitathmini kila siku juu ya biashara
yake na yeye mwenyewe kama yupo katika njia sahihi na kama amekosea wapi ili
ajirekebishe kukidhi matakwa ya biashara yake na mafanikio yake.
Ni laz\ima tuamue sasa kubadilika kwa kutafuta mafanikio na
sio kupenda mafanikio ukiyapenda bika kuwekeza katika kuyatafuta huenda
ukaishia kuwa mtu wakawaidza kama walivyo wengine ni lazima sasa uwe mbuni
miongoni mwa ndege ili utambulike na wanakuona.
Kuwa na wakati mwema na Mungu akubariki sana kwa kukubali
kupitia hapa princemedia tz
ASANTE KWA KUSOMA MAKALA HII UKIWA NA SWALI, MAONI AU USHAURI
USISITE KUWASILIANA NAMI
NGOBOLE, Andrea Ashery.
0755780131
facebook.com/ Andrea Ngobole
facebook page, instergram na twiter ni princemediatz
Post a Comment