Mbunge
wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo), amegonga mwamba baada ya
Kamati ya Kanuni ya Bunge kutoa msimamo wake kuhusu uchaguzi wa wabunge
wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA).
Hatua
hiyo inatokana na Zitto kuwasilisha barua kwa Spika wa Bunge, Job
Ndugai, Machi 28, mwaka huu akitaka kamati hiyo kutoa ufafanuzi wa
mgombe wa kundi C ili kila chama kiweze kushiriki uchaguzi, badala ya
kupewa kwa vyama vilivyokuwa na idadi kubwa ya wabunge.
Kutokana
na Tangazo la Bunge kwenye gazeti namba 11 la Machi 17, lililotangaza
uchaguzi huo na masharti yake, Zitto, alisema mwongozo wa uchaguzi huo
unavunja kanuni mbalimbali na kwamba kitakachofanyika sasa kitakuwa ni
uteuzi na si uchaguzi.
Alisema
pia mwongozo huo, mbali na kuvunja mkataba wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki, unaotaka suala la jinsi lizingatiwe kwenye wabunge
wanaokwenda kuiwakilisha nchi katika Bunge hilo, lakini pia inavinyima
vyama vingine vyenye uwakilishi bungeni haki ya kuchaguliwa.
Chanzo
cha kuaminika kimeema kuwa uamuzi huo ulifikiwa katika kikao cha
Kamati ya Kanuni, kilichokutana juzi mjini Dodoma chini ya Spika wa
Bunge, Job Ndugai, huku Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson akihudhuria.
Viongozi
wengine waliohudhuria kikao hicho ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani
Bungeni, Freeman Mbowe, Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba
Kabudi na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee.
Wengine
ni Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe pamoja na wajumbe kadhaa, ambapo
baada ya kufunguliwa kwa kikao hicho kilichomalizika usiku wa juzi,
Spika Ndugai, alihoji uhalali wa Zitto kuandika barua ya kuhoji mgawanyo
huo wa wabunge wa EALA.
“Kifupi
ni kwamba Zitto amekwama na hana tena namna maana Spika alimsema sana
kutokana na mgawanyo lakini kabla ya kuendelea zaidi kwamba alimuuliza
Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Kabudi kama kuna tatizo naye akasema
hakuna na Spika hajakosea.
“…
ila ni kikao ambacho Spika kwa kweli amesimamia sheria na ni kiongozi
asiyeyumba katika kusimamia sheria, sasa tunakwenda kwenye uchaguzi huku
ukweli ukiwa umeshajulikana, CCM watakuwa na viti sita, Chadema viwili
na CUF kimoja,” alisema mtoa habari huyo
Baaada
ya majadiliano ya kina na ufafanuzi wa kisheria kuhusu mgawanyo huo
wajumbe wa Kamati ya Kanuni walikubaliana na Spika Ndugai kwa kauli
moja, huku hoja ya Zitto ikitupwa na uchaguzi huo wa EALA utafanyika
kwa kuzingatia uwiano wa idadi ya wabunge wa vyama vyenye uwakilishi
bungeni.
Hata
hivyo kanuni ya 5(5) ya nyongeza ya tatu ya kanuni za Bunge inaeleza
“Chama chochote cha siasa chenye haki ya kusimamisha mgombea wa EALA
kinaweza kuweka wagombea watatu katika ya wagombea ubunge”.
Kutokana
na hilo msingi huo wa kikanuni inaonesha kuwa vyama vingine tofauti na
Chadema , CUF na CCM, haviwezi kusimamisha wagombea kwa sababu havikidhi
kigezo cha kanuni ya 12 za Kudumu za Bunge.
Post a Comment