Waziri
mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akimpongeza
mmoja wa wafanyabiashara wa kilimo cha pamba Riyaz Haider wakati wa
akitembelea maonesho ya mifuko ya uwezeshaji wananchi Kiuchumi, baada ya
mfanyabiashara huyo kupata mkopo kutoka katika benki kuu ya Tanzania
kupitia benki ya NMB.
Mfuko
wa Pensheni wa PPF unashiriki katika Maonesho ya Mifuko ya uwezeshaji
Wananchi kiuchumi kwa ajili ya kutoa elimu juu ya Mafao yanayotewa na
Mfuko huo.
PPF
inatoa Mafao mbalimbali na katika Maonesho haya unatoa elimu juu ya
mfumo wa ' Wote scheme' kwa sekta isiyo rasmi yaani wale wanaojiajiri
kama vile mama lishe, dereva boda boda, wakulima, wafugaji,
wajasiriamali, Wasanii, wote hawa wanathaminiwa na PPF ndio maana unato
fursa za huduma za afya, mikopo ya maendeleo, mikopo ya Elimu na Mafao
ya uzeeni.
Kupitia
Maonesho haya PPF inasajili wanachama wapya hapo hapo viwanjani pamoja
na kukabidhi vitambulisho vya uanachama wa Wote scheme.Hivyo ni fursa
muhimu kwa wakazi wa Dodoma kufika katika viwanja vya Maahujaa kupata
elimu hii muhimu na kujiunga na Mfuko huu ili kufaidika na Wote scheme.
Na kwa wale ambao hawapo Dodoma, wanaweza kutembelea Ofisi za PPF zilizopo karibu nao
Mkurugenzi
mtendaji wa asasi inayochochea uwekezaji sekta binafsi kwenye kilimo (
PASS ) Nicomedy Bohai akimuelezea mafanikio ya asasi hiyo Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa wakati wa maonesho ya
mifuko ya uwezeshaji Wananchi Kiuchumi yanayofanyika katika viwanja vya
mashujaa mkoani Dodoma.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akitoa cheti
kwa Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa udhamini wa Maonesho ya Mifuko ya
uwezeshaji Wananchi kiuchumi kwa Meneja wa PPF Kanda ya Mashariki na
Kati Michael Christian ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa PPF
William Erio, kushoto ni Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Sera
,Bunge, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu Mhe.Jenista Mhagama.
Mzee
Seleman Saleh akiwasikiliza Linda Mshana meneja wa mikopo kushoto na
Mary Kapeja mkuu wa kitengo cha masoko na biashara wa UTT Microfince PLC
kulia katika maonesho ya mifuko ya uwezeshaji Wananchi kiuchumi.
Enock
Humba, Afisa matekelezo wa bima ya afya na Grace Michael afisa masoko wa
elimu kwa umma wakitoa maelekezo wa watu waliotembelea banda la mfuko
wa bima ya afya katika viwanja ya mashujaa mkoani Dodoma.
Meneja
wa PPF wa Kanda ya Mashariki na Kati Michael Christian akimuelezea kazi
za PPF ikiwemo mafao yanayotolewa na Mfuko huo kama vile ' Wote scheme'
mmoja wa watu waliotembelea Maonesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi.
Afisa
Mfawidhi wa PPF Astro Liganga akimfafanulia Mkuu wa wilaya ya Shinyanga
Josephine Matilo fursa zilizomo ndani ya mfumo wa ' Wote scheme' wakati
alipotembelea banda la PPF katika Maonesho ya Mifuko ya uwezeshaji
Wananchi kiuchumi.
Moja
ya watu waliojitokeza katika maonesho ya mifuko ya uwezekezaji na uchumi
toka jamii ya wafugaji akiwa katika banda la PPF ambalo wameanzisha
mfumo unaotoa fursa kwa watu wote (hata wasioajiriwa) kuweza kuchangia
kima cha chini Tsh 20,000 kwa mwezi ambao utamwezesha mchangiaji kupata
mafao ya uzeeni na matibabu.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akiwa
katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa na wawakilishi wa Mifuko ya
uwezeshaji Wananchi kiuchumi mkoani Dodoma baada ya kufungua rasmi
Maonesho ya Mifuko ya uwezeshaji Wananchi kiuchumi.
Post a Comment