PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MOBISOL YAMPATA MSHINDI WA HAMASIKA NA MASIKA, AJINYAKULIA PESA TASLIMU
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Mshindi wa kwanza wa droo ya Hamasika na Masika Eliudi Yona aliyepo upande wa kulia mkazi wa maji ya chai mkoani Arusha akikabidhiwa kitit...
Mshindi wa kwanza wa droo ya Hamasika na Masika Eliudi Yona aliyepo upande wa kulia mkazi wa maji ya chai mkoani Arusha akikabidhiwa kitita cha shilingi laki mbili na mratibu wa masoko nchini wa kampuni ya mobisol Bwana Seth Gerald
NA: ANDREA NGOBOLE, PMT
Kampuni ya Sola ya mobinsol  nchini kupitia makao yake yaliyopo jijini Arusha,imetoa zawadi ya fedha taslimu laki mbili kwa mshindi wa kwanza wa droo ya kwanza ya hamasika na masika  bwana Eliud Yona ambaye ni mkazi wa maji ya chai


Akitaja washindi wapili na mshindi wa tatu,Mratibu wa masoko Seth Mathemu alisema kwa tukio kama hili pia fanyika mkoa wa Singida ambako mshindi wa pili Ally Suwedi amekabidhiwa radio inayotumia sola ya mobisol huku mshindi wa tatu kutoka Kilindi kampeni akikabidhiwa mashine ya kunyolea

Mratibu ,alisema mashindano ya msimu wa   Hamasika  Masika ,umegawanyika droo tatu,ambako droo ya kwanza mshindi alipatikana tarehe 22 aprili, na mashindano ya droo ya tatu kuanza Mei mosi ,na droo ya mwisho kufanyika Juni moja


Alisema pia mshindi atapatikana kutokana na kasi ya kushawishi wateja kununua mitambo yao ya sola,ambako kwa droo ya tatu mshindi wa kwanza atapata fedha taslimu, huku mshindi wa pili na wa tatu kupata zawadi za bidhaa zao,na katika droo ya mwisho mshindi wa kwanza atajipatia zawadi ya bodaboda kutoka kampuni hiyo

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top