Mara nyingi watanzania wamekuwa wanataja mafanikio ya nchi nyingine
wakilinganisha na mazingira hafifu ya hapa nchini katika masuala ya
Maendeleo.
Lakini orodha ya mazuri yanayoigwa na nchi nyingine kutoka Tanzania
itakuwa imeongezeka kwa jambo moja lingine ambalo ni Mabasi ya mwendo
kasi.
Aidha, Mamlaka ya usafiri jiji la Nairobi imefufua mpango kupunguza
foleni za magari kwa kuanzisha usafiri wa Mabasi ya Mwendokasi kama
yanayotumika kwa sasa nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa Katibu wa Masuala ya usafirishaji Mwangi Mariga alisema
ujenzi wa mradi huo wa Mabasi ya Mwendokasi utahusisha miji mitano.
Naye Katibu wa Baraza la Mawaziri James Macharia alishauri mwaka jana
kwamba mapendekezo maalum ya mfumo wa Mabasi ya usafiri yalikuwa na
changamoto kutokana na miundombinu iliyopo ya barabara kwa mabasi kuwa
na msongamano.
Mradi wa Mabasi ya Mwendokasi umebuniwa kufuatia idadi ya watu wa
Nairobi kuongezeka hadi milioni 3.3 kutoka 350,000 mwaka 1963 na idadi
ya magari inakadiriwa kufikia 300,000 bila ongezeko sawa katika mtandao
wa barabara.
Post a Comment