Watoto wa wafugaji wakiwa wanatizama Runinga ambapo taarifa ya habari ilikuwa hewani muda wa saa mbili za usiku baada ya kupelekewa umeme wa jua na kampuni ya Mobisol ambapo fursa hii itawawezesha watoto waliopo vijijini kutambua fursa za maendeleo nchini |
Kampuni ya Kimataifa ya umeme wa jua ya Mobisol ya Ujerumani, imetoa fursa kwa vijana wa vijijini ambao maeneo yao hayana umeme,kujiajiri katika kazi za kunyoa, kutokana na kuanza kusambaza mashine zinazotumia umeme wa jua huku ikitangaza kampeni ya kuhamasika na masika.
Akizungumza
katika ofisi ya mwananchi jana, Meneja masoko wa kampuni ya
Mobisol,Demetrius Wiston alisema, vijana wakitumia fursa zinazotokana na
kampuni hiyo,wataweza
kukabiliana na umasikini kwa kujiajiri wenyewe.
Alisema sambamba na huduma hiyo ya kunyoa, pia
kampuni hiyo imeanza kusambaza luninga zinazotumia jua ambazo zinaweza kutumika kibiashara, mitambo ya kuchaji
simu, radio na majokofu.
“huduma hii inapatikana katika mikoa 20 ambayo
tunafanya kazi na lengo letu kuwa ni kufika vijiji vyote, maeneo ambayo jamii
zipo nyuma”alisema
Kampeni ya hamasika na masika.
Katika hatua nyingine, Kampuni hiyo,imeanzisha
kampeni ya hamasika na masika, ambayo ina lengo la kuendesha bahati nasibu kwa
wateja wake watakaonunua bidhaa mwezi April na Mei katika mikoa
20 na zawadi zenye thamani ya milioni 4 zitatolewa.
Meneja chapa
na uwezeshaji wa Mobisol Seth Mathemu alisema zawadi mbali mbali ikiwepo fedha
taslimu,pikipiki na nyingine zenye thamani ya zaidi ya Sh 4 milioni zitatolewa.
Alisema mikoa ambayo itakuwa katika promosheni hiyo ni
Arusha, Kilimanjaro na Manyara,Singida, Dodoma, Tabora, Shinyanga, Mwanza,
Mara, Kagera, Simiyu, Geita, Kigoma, Rukwa, Iringa, Mbeya, Songwe, Njombe, Pwanipamojana Morogoro.
Post a Comment