Waziri
wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo (kushoto) akiwa katika
uzinduzi wa mradinwa usambazaji umeme vijijini (REA) awamu ya tatu
mkoani Mbeya leo.
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla (kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi
huo hii leo katika kijiji cha Ilinga, Wilayani Rungwe mkoani Mbeya.
Pamoja nae ni Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo.
VIJIJI 238 vya mkoa wa Mbeya vitanufaika na umeme wa REA awamu ya tatu imebainishwa.
Waziri
wa Nishati na madini Profesa Sospeter Muhongo ameyasema hayo hii leo
katika Kijiji cha Ilinga, Wilayani Mbeya wakati akizindua awamubya tatu
ya mradi huo wa kupeleka umeme vijijini.
Waziri
Muhongo amesema serikali imekusudia kupeleka Umeme katika Vijiji 12,000
katika awamu hii nchi nzima, na kuwawezesha wananchi kupata nishati
hiyo.
Akizungumza
na wananchi katika uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla
asema endapo Vijiji 238 vitapatiwa umeme kupitia mradi huo vitafanya
idadi ya vijiji vitakavyokosa umeme kuwa nane pekee.
"Endapo
awamu hii mtavipatia vijiji 238 umeme basi katika mkoa wangu ni vijiji
nane tu vitasalia, hivyo nawaomba na vyenyewe mviingize kwenye mradi ili
ifikapo 2020 Mkoa wa Mbeya usiwe na Kijiji kisichokuwa na
Umeme,"alisema Makalla.
Amesema
Mkoa wa Mbeya ni wazalishaji wakubwa wa chakula na uongezaji thamani
hivyo wa mazao ya kilimo hivyo umeme ni nishati muhimu ambayo
inahitajika mkoani humo.
Aidha
amenuomba Waziri Prof Muhongo na Shirika la Umeme nchini Tanesco
kushughulikia tatizo la kukatika mara kwa mara kwa umeme mkoani humo na
kuathiri shughuli za uzalishashaji viwandani, Uwekezaji na hata kwa
wananchi wa kawaida.
Katika
kutatua kero hiyo, Waziri wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo
amemuagiza Meneja wa Tanesco Kanda na Mkoa kushughulikia tatizo la
kukatika Umeme mara kwa mara.
Post a Comment