Akiwasilisha ripoti hiyo kwa Waziri Mkuu, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Profesa Samwel Mnyele alisema faru John alikosa matunzo na uangalizi wa karibu.
Mnyele ambaye ni Mkemia Mkuu wa Serikali alisema hakukuwa na kibali rasmi cha kumhamisha Faru John kutoka Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Grunet.
Alisema kamati hiyo imeshauri hatua za kiutawala zichukuliwe dhidi ya ofisi ya Mkurugenzi wa Wanyamapori na Mhifadhi wa Hifadhi ya Ngorongoro kutokana na mapungufu yaliyojitokeza.
Kwa upande wake, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipongeza kamati hiyo na kusema serikali itayafanyia kazi mapendekezo ili kulinda maliasili.
Chanzo: Mwananchi
Post a Comment