NA ESTOM SANGA-TASAF
Wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa
wametembelea kijiji cha Mlanda wilaya ya Iringa Vijijini mkoani Iringa
kukagua shughuli zinazotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF-
kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini-PSSN.
Wakiwa
kijijini hapo wajumbe wa kamati hiyo wameonyesha kuridhishwa kwao na
namna Mpango huo ulivyohamasisha wananchi kuboresha maisha yao ikiwemo
ujenzi wa nyumba za mabati,kusomesha watoto,kuanzisha miradi midogo
midogo ya kuichumi na kuboresha afya za familia za kaya hizo.
Akizungumza
na walengwa wa Mpango huo na viongozi, Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe.
Venance Mwamoto, ametaka serikali wilayani humo kuhakikisha kuwa
wataalamu wa ugani wanawatembelea walengwa wa Mpango huo kuwapa ushauri
wa namna bora ya kuendesha miradi wanayoianzisha.
‘’Tusiiachie
TASAF kwani nyie ndiyo mko karibu na walengwa hao,ili waweze kufanikiwa
zaidi wanahitaji hamasa na utaalamu wenu’’ alisisitiza Mhe. Mwamoto.
Kwa
upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki ametoa rai kwa watendaji
kuhakikisha kuwa watu wanaolipwa ruzuku ya TASAF ni wale tu waliokidhi
vigezo vya umasikini vilivyowekwa.
Aidha
Waziri Kairuki amesema ni dhamira ya serikali kuboresha maisha ya
wananchi ili kuwaondolea kero ya umasikini. Hata hivyo amesisitiza kuwa
walengwa wa Mpango huo waunde vikundi vya uzalishaji mali ili waweze
kunufaika na utaratibu wa mikopo inayotolewa na hivyo kukuza uwezo wao
wa kukopesheka.
Baadhi
ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za
Mitaa wakionyeshwa mabati aliyoyanunua mmoja wa walengwa wa Mpango wa
Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji cha Mlanda ,Iringa Vijijini ,Bi.
Konjeta Lyambafu aliyevaa kitambaa kichwani. Kushoto kwake Mwenyekiti wa
kamati hiyo Venance Mwamoto akimkabidhi fedha zilizochangwa na wajumbe
kuongeza uwezo wa mlengwa huyo kukamilisha mabati ili aezeke nyumba yake
iliyoko nyuma yao kwa bati.
‘’Ninaishukuru
serikali kupitia TASAF kwa kuniwezesha kuboresha maisha kwa kujenga
nyumba ya bati na kumudu kuwatunza na kuwasomesha wajukuu zangu wanane
’’ ndivyo mmoja wa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini Bi.
Claudia Kanyita mkazi wa kijiji cha Mlanda, wilaya ya Iringa Vijijini
anavyoelekea kuwaeleza wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Utawala
na Serikali za Mitaa pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki .
Mmoja
wa walengwa wa TASAF katika kijiji cha Mlanda wilaya ya Iringa Vijijini
Claudia Kanyita akiwa na wajukuu zake watatu alioachiwa baada ya watoto
wake kufariki, akitoa maelezo kwa kamati ya kudumu ya bunge ya Utawala
na Serikali za Mitaa iliyotembelea kijiji hicho kuona utekelezaji wa
Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na TASAF. Nyumba
inayoonekana nyuma yao imejengwa na Mlengwa huyo kwa ruzuku ya
TASAF.Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Ladislaus
Mwamanga.
Wajumbe
wa kamati ya kudumu ya bunge wavutiwa na jitihada za mlengwa wa TASAF
Bi.Claudia kijijini Mlanda na kumchangia fedha ili aanzishe mradi wa
kumwongea kipato, fedha hizo alikabidhiwa na Waziri Kairuki.
‘’Mgeni
njoo mwenyeji apone ’’ndivyo ilivyo kwa mlengwa wa Mpango wa Kunusuru
Kaya masikini wa kijiji cha Mlanda wilaya ya Iringa vijijini Konjeta
Lyambafu aliyechangiwa fedha na wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya
Utawala na Serikali za Mitaa ili aweze kuongezea fedha anazozipata
kupitia ruzuku inayotolewa na TASAF kuanzisha mradi wa kujiongezea
kipata. Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Venance Mwamoto akimkabidhi fedha
hizo mlengwa, kulia kwao ni Waziri Angellah Kairuki . Nyumba iliyoko
nyuma yao imeezekwa na mlengwa huyo kwa bati alizozinunua kupitia ruzuku
kutoka TASAF na hivyo kuboresha makazi yake.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti na Utumishi wa Umma na Utawala bora,
Angellah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na mmoja wa walengwa wa
Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na TASAF katika kijiji cha
Mlunda ,Iringa Vijijini, wakati kamati ya kudumu ya Utawala na Serikali
za Mitaa ilipotembelea kijiji hicho kukagua namna walengwa wa Mpango
huo wanavyonufaika na mpango huo.
Mwenyekiti
wa kamati ya kudumu ya Bunge Utawala na Serikali za Mitaa , Venance
Mwamamoto, Waziri Kairuki na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wakiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya
Masikini katika kijiji cha Mlanda , wilaya ya Iringa Vijijini wakati
kamati hiyo ilipofanya ziara kijijini hapo kuona namna walengwa wa
Mpango huo unaotekelezwa na TASAF wanavyonufaika na ruzuku itolewayo
kupitia mfumo wa Uhawilishaji fedha.
Wajumbe
wa kamati ya Kudumu ya bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakilakiwa
kwa shangwe na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini
unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii,TASAF,katika kijiji cha
Mlanda wilaya ya Iringa mkoani Iringa kuona namna walengwa hao
wanavyonufaika na fedha za Mpango huo.
Post a Comment