Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la kiserikali la Vision For
Youth Vaileth Ayoub akitoa maelezo juu ya Mradi wa Soko Mkononi,Picha na Woinde
Shiza
Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Zaidi ya
Wafanyabiashara 2000 wataweza kunufaika na Mradi wa soko mkononi unaotoa
taarifa za masoko na uwekezaji katika nchi za Afrika Mashariki.
Kutokana na
Changamoto ya Wafanyabiashara wa kati na wa wadogo kutokupata masoko mradi huo ulioko chini ya
Shirika lisilikoua la kiserikali la Vision for Youth umeanza kutoa taarifa za
masoko na fursa za uwekezaji.
Mkurugenzi
wa Shirika hilo Violeth Ayoub alisema
kuwa wanalenga nchi za Afrika
Mashariki ila kwa sasa wameanza na
Tanzania na Uganda ambapo kuna fursa nyingi za masoko na uwekezaji
ambazo hazijatumika huwezi kulinganisha na Kenya ukiangalia hata uchumi wake
umekua.
“Tumewalenga
Wanawake na Vijana kuelewa fursa zilizopo na kuzitumia vizuri kubadilisha
maisha yao na kufanikiwa kiuchumi” Alisema Vaileth
Mradi
unatekelezwa kwa njia tatu ikiwemo kuwa na kituo cha cha taarifa juu ya namna
ya kuingiza bidhaa ndani ya nchi na namna kupeleka bidhaa zako nje ya nchi
,sera za masuala ya biashara .
Mratibu wa
Mradi huo Janeth Nyambo anaeleza kuwa kwa sasa dunia imekua kama kijiji unaweza
kutumia simu yako ya mkononi kujua utawezaje kupata masoko ya biashara yako
,unaweza kuwekeza wapi badala ya kugombania fursa chache zilizopo.
Janeth
Alisema kuwa kwa wale Wabunifu walioko Tanzania wanaweza kubuni kitu ambacho
hakipo Uganda na wakapata fursa ya kukitangaza kupitia soko mkononi.
|
Post a Comment