Na Woinde Shizza,Arusha
Wanawake wote hapa nchini wametakiwa kujijengea tabia ya kupima afya zao mara kwa mara ili kuweza kujua matatizo ya mwili waliyonayo na kuyatatua kabla ya madhara makubwa kutokea .
Hayo yamebainishwa leo na mkurugenzi wa kampuni ya Phide entertaiment Phidesia Mwakitalima wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya wiki wanawake duniani ambayo inatarajia kuanza March mbili ambapo kwa mkoa wa Arusha maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika kwa muda wa siku saba katika viwanja vya kumbukumbu ya sheikh Amri Abeid .
Alisema kuwa wanawake wengi wamekuwa awana tabia ya kupima afya zao mara kwa mara kitu ambacho ni hatari mno kwani maisha ya sasa ukilinganisha na hali ya tabia nchi ilivyo pamoja na vyakula ambavyo vinaliwa kwa kipindi hichi.
Alisema kuwa kutokana na tatizo hilo kuonekana hivyo kampuni ya Phide entertaiment wameamua kuandaa kuandaa maadhimisho haya kwa kuwapa fursa wanawake kujitokeza kupima afya zao bure ambapo alisema tukio zima litafanyika katika viwanja vya kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid kwa muda wa siku saba ambapo alisema kuwa maadhimisho haya yataanza rasmi March 2 hadi March nane.
" tamasha hili kubwa linawapa fursa wanawake kuweza kupima Afya yako bure na magonjwa ambayo yatapimwa katika wiki hii ni pamoja na Moyo, Kisukari, Macho, na figo hivyo napenda kuwasihi wanawake wenzangu wote wajitokeze kwa wingi waje wapime afya zao na wajijue vizuri "alisema Phide
Aidha alisema kuwa mbali na kupima afya pia wiki hiyo itatumika kwa ajili ya kuwapa wanawake ushauri juu ya kupima afya zao mara kwa mara ambapo watawapa elimu ya kutosha .
"unajua kipindi hichi wanawake wamekuwa wanapata magonjwa ya haina mbalimbali na wingine wamekuwa wanapuuzia kwenda hospitali kupima afya zao mara kwa mara hivyo tamasha hili la wiki nzima litatumika kuwaelimisha wanawake faida za kupima afya zao mara kwa mara"alisema Phide
Alimalizia kwa kuwataka wanawake wote kutopuuzia wiki hiii kwani ni muhimu sana kwa kujotokeza kupima afya zao na wajue mfumo mzima wa miiili yao ilivyo pamoja na kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya .
Post a Comment