PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Askofu Gwajima: Makonda ni Kombora Ambalo Halijaelekezwa pa Kutua, linaweza Kutua Sehemu Yoyote!
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Askofu Josephat Gwajima amesema akimpeleka Makonda mahakamani, atakuwa amepeleka serikali mahakamani. Hivyo atamshtaki Makonda kwa R...


Askofu Josephat Gwajima amesema akimpeleka Makonda mahakamani, atakuwa amepeleka serikali mahakamani. Hivyo atamshtaki Makonda kwa Rais ili achukue hatua zinazostahili na hatokubali akiendelea kuwa mkuu wa mkoa.

Gwajima amedai watu wasiwalaumu jeshi la polisi kwani na wenyewe wanateswa kama wanavyoteswa wao. Amesema alipoenda polisi amekuta nao wameswekwa ndani kwa amri ya Makonda. Amedai matatizo yote yamesababishwa na 'kiumbe mmoja'.

Amempongeza Rais kwa kumchagua mkurugenzi husika na amemshauri asiache kuamini vijana kwa kuwa kijana mmoja ameharibu.

Baadhi ya Maneno yake Haya Hapa:

Gwajima: Lengo la Paul Makonda ni kuchafua majina ya watu kwa sababu anazozijua mwenyewe.

Askofu Gwajima: Askari walipekuwa nyumba yangu chumba hadi chumba lakini hawakukuta kitu chochote.

Askofu Gwajima: Mimi nitawaambia kitu, msilaumu Polisi wala Ofisi ya Rais. Wao hawahusiki na hili ila ni kiumbe mmoja tu ameibuka katikati.

Askofu Gwajima: Waliniambia wakanipime kwa Mkemia na walinipima kwa uwazi kabisa. Niliwaambia hata wakikuta pombe wasema ni dawa za kulevya.

Askofu Gwajima: Polisi nao wanateswa kama tunavyoteswa sisi. Wanaambiwa wakapekuwe nyumba yangu japo wanajua hamna kitu ila inabidi waende.

Askofu Gwajima: Baada ya kukosa walichokuwa wanatafuta nyumbani kwangu tukarudi polisi usiku ule ule kuendelee na mahojiano.

Askofu Gwajima: Kamanda Sirro akaniuliza kwa nini nimewekwa kwenye orodha hiyo, nikamwambia ni chuki tu za mtu aliyekaa kwenye kiti chake.

Askofu Gwajima: Sijawahi kuvuta sigari, kunywa pombe wala kwenda disko tangu nimezaliwa mimi.

Gwajima: Chumba nilichowekwa polisi nilikuwa mimi na manji. Nikasema 'kumbe na mimi nina pesa kiasi hiki hadi nawekwa na huyu?'

Askofu Gwajima: Kwanini kina Manji wao hadi leo hawajafanyiwa kama nilivyofanyiwa mimi ili nao watoke mule ndani?

Askofu Gwajima: Manji ana kampuni 23, na ameajiri watu zaidi ya 5000. Unashindwaje kumpelekea hati ya kumuita umhoji kabla ya kumtangaza?

Askofu Gwajima: Baada ya kukosa madawa, utalisafishaje jina langu nililolijenga kwa jasho kubwa kwa miaka 29?

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top