PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Yanga ya Lwandamina Yavunja Mwiko wa Miaka 30 Kwa Staili Hii Mpya..!!!
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Goli la mshambuliaji Deus Kaseke limeivunja Yanga kuvunja mwiko wa miaka 30 zaidi  katika uwanja wa M...


 

Goli la mshambuliaji Deus Kaseke limeivunja Yanga kuvunja mwiko wa miaka 30 zaidi  katika uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma na kuondoka na alama tatu muhimu mchezo wa Ligi kuu Vodacom Tanzania bara dhidi ya wenyeji Majimaji.


Dakika ya 14 Kaseke alifunga goli baada ya mlinda mlango wa Majimaji kuutema Mpira uliokuwa umepigwa na Nahodha wa Yanga Haruna Niyonzima na kumkuta mfungaji akiwa katika hali nzuri na kuweza kutikisa nyavu za wenyeji.

Simon Msuva na Amis Tambwe wangeweza kufunga magoli mengi zaidi kutokana na kukosa nafasi nyingi za wazi hadi Mapumziko Yanga walienda wakiwa kifua mbele kwa goli hilo moja.

Kipindi cha pili kilikuwa kigumu kwa kila timu na kupelekea kufanya mabadiliko mbalimbali huku Yanga wakicheza kwa kushambulia na kukaba zaidi kutokana na Mpira kukosa radha kutokana na ubovu wa uwanja huo.

Mpaka dakika 90 Mwamuzi Hussein Athumani anapuliza kipyenga cha mwisho Yanga wameibuka na pointi tatu muhimu na kuweza kumsongelea mtani wake Simba ambaye anaongoza Ligi Kuu.

Kwa Matokeo hayo Yameifanya Majimaji kuwa katika Mstari wa kushuka daraja hivyo wanatakiwa kubadilika kwa mechi ambazo zimebaki wakati Yanga wamefikisha pointi 43 nyuma ya moja dhidi ya Simba wenye 44.

Ligi Kuu ya Tanzania inatarajia kuendelea tena kesho kwa michezo miwili kucheza katika viwanja mbalimbali macho ya wengi yatakuwa mkoani Morogoro Mtibwa Sugar watawakaribisha Vinara wa Ligi timu ya Simba wakati Mabingwa wa Kombe la Mapinduzi Azam FC watacheza na Mbeya City majira ya saa moja usiku kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

Kikosi cha Yanga ; Deogratius Munish ‘Dida’, Juma Abdul, Haji Mwinyi, Andrew Vincent, Kelvin Yondani, Thaban Kamusoko, Simon Msuva, Haruna Niyonzima/Oscar Joshua dk90, Amissi Tambwe, Juma Mahadhi na Deus Kaseke/Said Juma ‘Makapu dk’80.

Maji Maji; Agathon Anthony, Salehe Mohammed, Mpoki Mwakinyuke, Keneddy Kipepe, Bahati Yussuf/Emmanuel Semwanza dk25, Yakoub Kibiga/Paul Nyangwe dk58, Iddi kipwagile, Kelvin Kongwa, George Mpole, Hassan Hamisi na Lucas Kikoti/Peter Mapunda dk46.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top