PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Rais Trump Atumia Barua ya Obama Kukejeli Wanahabari..!!!
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
RAIS wa Marekani, Donald Trump, ameendelea kuwashambulia waandishi wa habari, safari hii akiwakejeli kwa ‘kuwaringishia’ barua aliy...

RAIS wa Marekani, Donald Trump, ameendelea kuwashambulia waandishi wa habari, safari hii akiwakejeli kwa ‘kuwaringishia’ barua aliyoandikiwa na mrithi wake katika Ikulu ya White House, Barack Obama, akiwaambia licha ya kiu ya habari waliyokuwa nayo, hatafichua ujumbe uliomo kwenye barua hiyo.

Kwa kawaida nchini Marekani, rais anayeondoka madarakani humuandikia ujumbe wa barua rais mpya, ujumbe ambao hubeba mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na ushauri unaozingatia uzoefu wa mhusika katika Ikulu ya nchi hiyo.

“Ile nimefika tu ofisini Ikulu nikaikuta barua hii (anaionyesha kwa waandishi) iliyoandikwa kwa umahiri mkubwa kutoka kwa rais Obama,” Trump aliwaeleza waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wake huo, kisha akaongeza; “Ni uungwana wa hali ya juu kwake kuniandikia barua hii, kwa kweli tunaenzi ujumbe wake. Tutaufanyia kazi ujumbe huo na vile vile hatuwezi kufichua ujumbe husika kwenu waandishi wa habari.”

Wakati Obama akiingia madarakani, katika Ikulu ya White House aliachiwa barua na mtangulizi wake, George W. Bush. Katika barua hiyo, pamoja na mambo mengine Bush aliandika akimwambia Obama kwamba kutakuwa na nyakati za “majaribu” ya kiuongozi katika kipindi chake akiwa madarakani. Vile vile Bush, kupitia ujumbe wa barua hiyo alimuonya Obama kwamba kutaibuka wimbi la wakosoaji dhidi yake.

“Mungu atakuwa upande wako kwa ajili ya kukupa faraja. Katika mkondo huo wa faraja, mapenzi ya kifamilia yatakuwa upande wako, nchi yako haitakutupa, ikiwa ni pamoja nami,” aliandika Bush.

Lakini si tu barua ya Bush kwa Obama ndio iliyowekwa wazi kwa waandishi wa habari bali pia barua iliyoandikwa na rais Bill Clinton kwa aliyekuwa mrithi wake Ikulu, rais Bush.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top