PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Mwana FA ataja wasanii ambao hatafanyanao kazi
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Rapa Mwana FA ambaye kwa sasa anafanya vyema na ngoma yake 'Dume Suruali' amefunguk...


Rapa Mwana FA ambaye kwa sasa anafanya vyema na ngoma yake 'Dume Suruali' amefunguka na kuweka wazi kuwa hana mpango kwa sasa kufanya kazi na wasanii kama Lady Jaydee, Prof Jay, Juma Nature na wengine wengi.
Mwana FA

Mwana FA alisema haya kupitia kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kusema kwa sasa hana mpango wa kufanya kazi na wasanii wengi tu lakini kutofanya nao kazi haina maana kuwa ana matatizo nao.
"Kwa sasa sina mpango wa kufanya kazi na Lady Jaydee, harafu hili swali limekuwa likijirudia sana sina mpango wa kufanya kazi na Prof Jay, Juma Nature na wasanii wengine wengi tu, lakini sina tatizo nao na wala sina tatizo na yoyote kati yao" alisema Mwana FA 
Mbali na hilo Mwana FA anasema anafurahi kuona muziki wa hip hop nchini sasa umegeuka na kufanya vizuri zaidi kuliko hata ngoma za wasanii wa kuimba na kusema hiyo ni dalili kuwa wanamuziki wa hip hop wamegundua sehemu walipokuwa wakikosea. 

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top