PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: LEMA, MKEWE KUPANDISHWA KIZIMBANI KUJIBU KESI YA KUMTUSI GAMBO
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, Augustino Rwezile, leo, anatarajia kuwasomea hoja za awali Mbunge wa Arus...
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, Augustino Rwezile, leo, anatarajia kuwasomea hoja za awali Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless  Lema na mkewe, Neema katika kesi inayowakabili ya kumtukana Mkuu wa mkoa huo, Mrisho Gambo.

Hoja hizo ilikuwa wasomewe Novemba 15, 2016 lakini zilikwama kusomwa kutokana na Lema kuugua ghafla na Wakili wa Serikali, Elizabeth Swai kumuomba hakimu kutumia busara ya Mahakama kuisogeza mbele kesi hiyo kutokana na hali ya mbunge huyo.
Lema bado anasota rumande kwa siku 76 tangu Novemba 2, mwaka jana baada ya kukosa dhamana katika kesi inayomkabili ya tuhuma za kutumia lugha ya uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli.
Kutokana na sababu hiyo, Hakimu Rwezile pia amwahirisha kesi ya kuhamasisha maandamano ya Ukuta inayomkabili mbunge huyo na ile ya kumtumia ujumbe mfupi wa maneno Gambo unaodaiwa kuwa na matusi hadi leo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top