Shirikisho la Soka nchini TFF
limesema, kuachana na aliyekuwa Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania
“Taifa Stars” Charles Boniface Mkwassa “Master” ni makubaliano ya
kimkataba kwa pande zote mbili na hakukuwa na tofauti zozote
ziliyojitokeza.
Boniface Mkwasa
Afisa
habari wa Shirikisho la Soka nchini TFF Alfred Lucas amesema,
wanatarajia kumalizana kabisa na Mkwasa mpaka ifikapo mwezi wa Machi
mwaka huu ikiwemo fidia za kukatisha mkataba.
Alfred amesema, wataendelea kufuata program aliyoiacha Mkwasa huku wakitumia pia programu ya Kocha Salum Mayanga ambaye atakuwa na jukumu la kuandaa kikosi cha wachezaji wa ndani kwa ajili ya hatua ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi ya ndani (CHAN).
Mkwasa alichukua mikoba kutoka kwa kocha Mart Nooij raia wa Uholanzi ambaye alifundisha tangu mwaka 2014 hadi 2015.

Salum Mayanga - Kocha mpya Taifa Stars
Kocha Salum Mayanga anachukua nafasi ya Kocha Charles Boniface Mkwasa
ambaye mkataba wake unafikia mwisho mwezi wa Machi, mwaka huu ambapo
kati ya majukumu yake yatakuwa ni kuandaa kikosi cha timu ya Taifa kwa
ajili ya hatua ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 ambazo
mechi za awali zitaanza mapema mwaka huu.
Post a Comment