Mwanamuziki Ben Pol
amefunguka na kuweka wazi ukweli kuhusu tuhuma za yeye kuiba Idea ya
wimbo wa 'Phone' ambao amefanya na Mr Eazi
Ben Pol
Ben Pol amesema katika wimbo wake wa
'Phone' Verse ameandika yeye neno kwa neno na sehemu ambayo ameimba Mr
Eazi ameandika Eazi mwenyewe na kusema katika wimbo huo Producer Tiddy
Hotter alimpa Idea ile ya 'Baby oohh why you check my phone' ambayo
ndiyo Sappy amekuwa akisema ya kwake.
"Unajua saizi mimi nafanya kazi na Tiddy
Hotter siku moja akaniambia Ben Pol kuna beat moja nataka kukupa sijui
na wewe utaipotezea kama wengine? Nikamwambia nipe na wakati ananipa ile
beat tayari yeye alikuwa amefanya chorus hivyo mimi nikaandika verse
mbili na kufanya baadaye alivyokuja Mr Eazi niliitoa verse moja na
kuongezea jambo kwenye chorus ile" alisema Ben Pol
Ben Pol anadai producer Tiddy Hotter
alimsisitiza sana kuhusu kazi hiyo na kumtaka ifanyie kazi siyo kama
wengine ambao amekuwa akiwapa idea harafu wanashindwa kuzifanyia kazi
idea hizo.
"Kiukweli Tiddy Hotter alipokuwa ananipa
hiyo beat alisisitiza sana kuifanyia kazi na nikaifanyia kazi ila
nachoweza kusema Sappy namwambia afanye kazi aache mambo ya kiki
hayawezi kumsaidia maana huyo Sappy nilishawahi kufanya naye kazi nikiwa
na Nameless lakini akaivujisha kazi yangu, hivyo aache ujanja ujanja
apige kazi mbona wenzake kina Nahreel, Mensen Selekta wanapiga kazi na
kazi zao zinasikika aache maisha ya kiki. Kwangu mimi hili alilofanya
halijaniathiri kabisaa kwanza ndiyo nimeongeza downloads kwangu kwa hiyo
mtu anaye loose ni yeye" alisema Ben Pol
Post a Comment