Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitembelea Mradi wa umwagiliaji katika kijiji cha Jobag wilaya ya Karau ,mradi uliojengwa kwa ufadhili wa shirika la Worl Vision |
Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Waziri Mkuu
wa Tanzania Kassim Majaliwa amezindua mradi wa Umwagiliaji katika kijiji cha
Jobag wilaya ya Karatu uliofadhiliwa na Shirika la Worlvision ambao unahudumia
ekari 1200 na kuwafikia wakulima 4000.
Akizungumza
katika uzinduzi wa Mradi huo ,Majaliwa amesema kuwa mradi huo utasaida
kuchochea kilimo cha umwagiliaji hasa katika kipindi hiki ambacho kuna
mabadiliko ya tabia ya nchio na uhaba wa mvua.
Majaliwa
amesema kuwa Asilimia 80% ya Watanzania wamejiajiri katika sekta ya kilimo
idadi ambayo ni kubwa hivyo kilimo cha umwagiliaji kikihamasishwa ipasavyo
wakulima watapata tija kubwa na kuinua pato la taifa.
Aidha
amelishukuru shirika la Word vision kwa kujitoa kusaidia jamii katika eneo hilo
muhimu la kilimo ambalo ni tegemeo kwa wakulima wengi.
Waziri Mkuu
ameonya tabia ya baadhi ya watu wanaohujumu vyanzo vya maji kwa kuunganisha
mashine katika vyanzo na kufanya uharibifu hivyo amewataka kuondoka mara moja
katika chanzo hicho na iwapo watakaidi serikali itawachukulia hatua kali.
Mkurugenzi
wa Miradi katika shirika la World Vision Revocatus Kamara amesema kuwa mradi
huo utawanufaisha wakulima wengi na kupelekea upatikanaji wa chakula pamoja na
kukuza kipato cha wakulima.
Kamara
amesema kuwa shirika hilo litaendelea kushirikiana vyema na serikali ili
kufanya miradi itakayosaidia kutatua changamoto zinazoikabili jamii.
Post a Comment