Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
ameitaja rushwa kama changamoto sugu ambayo bado inaendelea kulitafuna
taifa la Tanzania katika miaka yake 55 ya Uhuru.
Rais Magufuli ameitaja changamoto hiyo wakati akiwaongoza watanzania
katika maadhimisho ya miaka 55 ya uhuru wa Tanzania Bara ikiwa ni mara
ya kwanza tangu aingie madarakani na kutaja changamoto nyingine kuwa ni
tatizo la ajira pamoja na umasikini.
Akizungumza katika hotuba yake ya shukrani katika maadhimisho hayo
ambayo yamefanyika katika uwanja wa uhuru jijini Dar es Salaam, Dkt.
Magufuli, amesema kuwa serikali yake itaendelea kupambana na vitendo na
rushwa na ufisadi, kwa ajili ya kuliletea taifa maendeleo.
Aidha Rais Dkt. Magufuli amesema kuwa serikali itahikisha kuwa inaondoa
uonevu hasa kwa wananchi wanyonge ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto
zinazowakabili ili kila mtanzania aweze kufaidika na matunda ya nchi
yake.
Maadhimisho hayo ambayo kwa mujibu wa Rais Magufuli ndio ya mwisho
kufanyika Jijini Dar es Salaam na kuanzia mwakani yataadhimishwa Dodoma,
yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wastaafu na serikali pamoja na
mabalozi wa nchi mbalimbali zenye uwakilishi hapa nchini.
RUSHWA YAZIDI KUMTESA RAISI MAGUFULI
Title: RUSHWA YAZIDI KUMTESA RAISI MAGUFULI
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameitaja rushwa kama changamoto sugu ambayo bado inaendele...
Post a Comment