PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Lori Lamuua Padri Saa 6 Kabla ya Krismasi
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Watu hao walikumbwa na mauti, baada ya lori moja la kusomba mawe, kokoto na mchanga kuparamia gari dogo aina ya Toyota H...


Watu hao walikumbwa na mauti, baada ya lori moja la kusomba mawe, kokoto na mchanga kuparamia gari dogo aina ya Toyota Hilux, mali ya Kanisa Katoliki lililokuwa likiendeshwa na Padri Andrew Lupondya (35) wa Parokia wa Kanisa Katoliki Jimbo la Kahama mkoani Shinyanga.

Ajali hiyo ilitokea juzi saa tisa alasiri zikiwa ni saa sita kabla kuanza misa ya mkesha wa Krismasi ambayo kwa mujibu wa taratibu za Kanisa Katoliki huanza saa 3 usiku.

Watu wanne walifariki papo hapo katika eneo la tukio la Kanegele Kata ya Masumbwe wilayani Mbogwe mkoa wa Geita, katika barabara kuu kutoka Isaka kwenda Lusahunga na nchi jirani ya Rwanda, akiwamo Padri Lupondya huku watu wengine wanne wakijeruhiwa.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top