Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Benki ya KCB
nchini Tanzania imetoa msaada wa kiasi cha fedha cha shilingi Milioni 48 kwa
ajili ya ujenzi wa Vituo vya kunawa mikono vinavyojulikana kama Hand washing
station katika shule za Mairowa
Intergrity na Kondoa Intergrity zilizoko chini ya taasisi ya Ereto East Africa Foundation.
Akizungumza
katika hafla ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika katika ofisi za benki hiyo ,Meneja wa Benki hiyo Tawi la Arusha Hogla Laizer amesema kuwa msaada huo ni moja
kati ya mchango wa benki hiyo kwa jamii hususan katika suala la elimu na afya
hasa katika maeneo yenye changamoto kubwa ya maji .
Meneja huyo
amesema kuwa msaada huo tayari umezisaidia shule za Kondoa Intergrity na
Mairowa Intergrity zilizoko chini ya Ereto East Africa Foundation .
“Katika
kuchangia elimu Benki ya KCB kwa kipindi cha miaka mitatu imetoa misaada ya
thamani ya shilingi milioni 300 ili kuboresha elimu kwa kutoa madawati na vifaa
vingine vya kuboresha huduma za elimu” Alisema Hogla
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Ereto East Africa Foundation Bwana Godsave Ole Megiro amesema
kuwa msaada huo utasaidia kutatua tatizo la magonjwa ya matumbo na kipindu
pindu yanayotokana na kutokunawa mikono kwa kuanzishwa kwa vituo hivyo vya
kunawa mikono.
Godsave
amesema kuwa wameweka vituo hivyo karibu
na vyoo na karibu na mabwalo ya kunawa mikono jambo ambalo limepunguza idadi
kubwa ya wanafunzi waliokuwa wakiugua magonjwa ya matumbo.
Post a Comment