BASI LA KANDAHAR LAGONGA LAUA ARUSHA
Basi la Kampuni ya Kandahar kama linavyoonekana pichani( Picha pamoja na habari na Vero Ignatus Blog)
Na.Vero Ignatus Arusha.
Basi la kampuni ya Kandahari T 785 DFM limemgonga mtembea kwa miguu na kusababisha kifo chake papo hapo.
Akizungumzia mazingira ya ajali hiyo Kamanda wa polisi mkoani Arusha Charles Mkumbo amesema ajali hiyo imetokea leo majira ya saa sita na nusu mchana Jijini hapa.
Amesema kuwa basi hilo lilikuwa linatokea Moshi kuelekea singida lakini lilipofika Arusha kwenye kivuko cha watembea kwa miguu chini ya mti ( zebra crossing ) dereva alikaidi kusimama ili watembea kwa miguu wavuke ndipo aliposabababisha kifo cha mtoto huyo.
"Dereva huyo alifika zebra crossing hakusimama kuna mama alikuwa anavuka pamoja na mwanae, mama yeye alifanikiwa kukimbia lakini mtoto aligongwa na kufariki papo hapo"alisema kamanda.
Aidha amemtaja dereva aliyekuwa anaendesha basi hilo kuwa ni Immanuel Nyari miaka( 46) mkazi wa mbauda jijini hapa ,pamoja na jina la marehemu ni Ezra Samson miaka (7) mkazi wa Sombetini.
Kamanda Charles Mkumbo amewataka madereva waheshimu na kuzingatia sheria za usalama barabarani ikiwemo kwenye vivuko,madaraja,kwenye kona huku wakitambua kuwa hawatumii barabara peke yao.
Amesema madereva ambao watakiuka kuheshimu na kuzingatia sheria za usalama barabarani watawachukulia hatua kali za kisheria pamoja na kuwanyang'anya leseni
Post a Comment