mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo anazindua daraja ambalo limejengwa na wawekezaji lililogarimu zaidi ya shilingi milioni 65 za kitanzania
Mkuu wamkoa wa Arusha akiwa anaongea na wananchi wa kata ya Engutoto ilipo ndani ya jiji la Arusha
wa kwanza kulia ni muwekezaji
Hans Paul katikati ni mkuu wa mkoa wa Arusha mrisho Gambo kushoto ni mkurugenzi wa jiji la ArushaAthuman Kiamia wakipiga magofi mara baada ya kuzindua daraja
Hans Paul katikati ni mkuu wa mkoa wa Arusha mrisho Gambo kushoto ni mkurugenzi wa jiji la ArushaAthuman Kiamia wakipiga magofi mara baada ya kuzindua daraja
Na Woinde Shizza,Arusha.
Wananchi wa Kata ya Engutoto jijini
Arusha wamelalamikia uuzaji holela wa maeneo ya wazi ya serikali hali
inayopelekea uhaba wa maeneo ya kujenga huduma za kijamii kama zahanati na
shule huduma ambazo hazipatikani katika kata hiyo hivyo wameiomba serikali
itatue tatizo hilo ili wananchi wapate huduma bora za kijamii.
Wakitioa malalamiko yao mbele ya
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo wamesema kuwa licha ya uuzaji holela wa
ardhi kuna migogoro ya ardhi katika kata hiyo na wananchi wengi
wanaomiliki ardhi bado hajapatiwa hati jambo ambalo linawapa wasiwasi kuwa
huenda ardhi zao zikamegwa na wawekezaji
Mmoja wa wananchi hao
aliyejitambulisha kwa jina la Joseph
Kamete alisema kuwa wameomba sana hati za maeneo ambayo wanaishi lakini
wamekuwa awapewi na wanazungushwa zungushwa kitu ambacho kinawatia mashaka makubwa.
“mkuu wa mkoa kinachotuuma zaidi sisi tumekaa
hapa tangu kipindi cha mikonge lakini tukiomba hati hatupewi lakini akija
muwekezaji anapatiwa hati kwa wakati sasa tunajiuliza inamaana sisi atuna haki
ya kukaa katika viwanja hivi watuambie tu ili na sisi tujue sio wanafanya kazi
ya kutuzungusha zungusha kwakweli tumekuwa tunaishi kama ndege katika maeneo
yetu na atuna amani kabisa maana kama wanatunyima hati wanania gani kweli
tunaomba mkuu wa mkoa utusaidie kwa hili “alisema Zaituni Marunda
Aidha wananchi hao pia wanasumbuliwa
na kero za maji na umeme kwa kipindi kirefu hivyo wameiomba serikali
iwasaidie kutatua kero hiyo inayowaathiri zaidi kinamama ambao hutembea umbali
mrefu wakitafuta huduma za maji
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo
ambaye alifika katika kata hiyo katika shughuli ya uzinduzi wa daraja
lililojengwa na mwekezaji Hans Paul ameagiza ofisi ya Mkurugenzi kumkabidhi
ripoti ya maeneo ya wazi ya jiji yaliyouzwa kienyeji ili aweze kushughulikia
kero hiyo pia ameshukuru kampuni ya Hanspaul kwa kujitoa kusaidia jamii
jambo ambao linapaswa kuigwa na wawekezaji wengine
Alisema kuwa wao kama serikali wapo
tayari kushirikiana na wawekezaji ambao wanalipa kodi kama ipasavyo na wale
ambao wanajishuhulisha katika kusaidia jamii inayowazunguka.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha amefanya mkutano
wa kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi pamoja na kuzindua daraja
ambalo limegharimu kiasi cha shilingi milioni 67.
Post a Comment