|
Mkuu wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha (AJTC) Andrew
Ngobole akizungumza katika Mahafali ya Chuo hicho ambapo Wanafunzi
wametunukiwa vyeti vya Shahada na Stashahada.Picha na Ferdinand Shayo |
|
Mkurugenzi wa Mafunzo wa Chuo cha Arusha Journalism Training College
(AJTC) Joseph Mayagila akizungumza katika Mahafali ya chuo hicho
yaliyofanyika
chuoni hapo,wapili kutoka kushoto ni Meya wa Jiji la Arusha Kalisti
Lazaro,wakwanza kushoto ni Diwani wa kata ya Themi ,Melans Kinabo na
kulia ni Mkurugenzi wa Safina Radio Elifuraha Samboto Picha na Ferdinand
Shayo Picha na Ferdinand Shayo |
|
Meya wa Jiji la Arusha Kalisti Lazaro akimtunuku cheti cha stashahada ya
Uandishi wa Habari na Utangazaji Amani Mmbando wa Chuo cha Arusha
Journalism Training College
(AJTC),wawatu kulia ni Mkurugenzi wa Mafunzo wa Chuo cha Arusha
Journalism Training College
(AJTC) Joseph Mayagila.Picha na Ferdinand Shayo |
|
Meya wa Jiji la Arusha Kalisti Lazaro akimtunuku cheti cha stashahada ya
Uandishi wa Habari na Utangazaji ANASTAZIA ELIASI wa Chuo cha Arusha
Journalism Training College
(AJTC),wawatu kulia ni Mkurugenzi wa Mafunzo wa Chuo cha Arusha
Journalism Training College
(AJTC) Joseph Mayagila.Picha na Ferdinand Shayo |
|
Meya wa Jiji la Arusha Kalisti Lazaro akikabidhiwa Zawadi
na
Mkurugenzi wa Mafunzo wa Chuo cha Arusha Journalism Training College
(AJTC) Joseph Mayagila katika Mahafali ya chuo hicho yaliyofanyika
chuoni hapo.Picha na Ferdinand Shayo |
|
Meya wa jiji la Arusha Kalisti Lazaro akizungumza katika Mahafali ya
Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha (AJTC) ,Kulia ni
Mkurugenzi wa Mafunzo katika Chuo hicho Joseph Mayagila,kushoto ni
Diwani wa kata ya Themi ,Melans Kinabo.Picha na Ferdinand Shayo |
|
Mkuruf=gezi mtendaji wa mafunzo wa AJTC akitoa hotuba ya katika mahafali hayo na kumkaribisha mgeni rasmi ili aweze kuwatunuku vyeti wahitimu |
|
Wahitimu wa chuo hico wakirusha kofia juu na kushangilia mara baada ya kutunukiwa diploma ya uandishi wa habari ya chuo cha uandishi wa habari Arusha |
|
picha ya pamoja na wahitimu
|
Na Ferdinand Shayo,Arusha .
Meya wa Jiji
la Arusha Kalisti Lazaro amewataka wanahabari nchini kuhakikisha wanatumikia jamii masikini isiyosikika ili kuikwamua na matatizo yanayoikabili.
ameyasema hayo alipokuwa akiwatunuku diploma ya uandishi wa habari zaidi ya wahitimu 50 waliohitimu katika
Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji
(AJTC) huku akiwataka kuwa mstari wa mbele katika kupigania haki za
jamii na kuleta mabadiliko kupitia kalamu zao.
Kalisti
amewataka Wanahabari kujikita katika kuandika habari za kijamii zitakazosaidia
kutatua changamoto zinazoikabili jamii na kuleta suluhu kwenye matatizo ya
jamii.
Aidha kutokana na kupitishwa kwa sheria mpya ya habri Ameishauri serikali
kuangalia upya mswada wa habari na kuufanyia marekebisho katika vipengelea
ambavyo vinaminya haki ya habari.
Naye Mkurugenzi
wa Mafunzo katika Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji ,Joseph Mayagila
amesema kuwa tasnia ya habari ni tasnia muhimu katika kuchochea maendeleo ya
nchi kwani bila taarifa hakuna maendeleo.
Alisema kuwa
ni vyema serikali ikatazama upya utekelezaji wa sheria mpya na kufanyia kazi
mapungufu ili wanahabari waendelee kuwahabarisha Watanzania.
Post a Comment