PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MAKALA: INUKA UANGAZE UFANIKIWE KIMAISHA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Na Ferdinand Shayo,Arusha. Kila mtu duniani   ana mwanga ndani yake ama nuru ya aina fulani ambayo amekuja nayo duniani ili kuianga...
Image result for FERDINAND SHAYO

Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Kila mtu duniani  ana mwanga ndani yake ama nuru ya aina fulani ambayo amekuja nayo duniani ili kuiangaza dunia.

Mwanga  ulionao ni mithili ya taa ,taa yako inaweza kuwa kipaji ulichonacho ,ubunifu ama uwezo ulionao ambao unaweza kukutoa kwenye giza la umasikini.

Wangapi wana taa ndani yao na bado wanaishi kwenye giza totoro la umasikini,maradhi na ujinga.

Pengine una taa ndani yako ila hujui namna ya kuiwasha ili ujiangazie na kuwaangazia wengine ndio maana uko gizani.

Gundua taa yako ni ipi,itumie kujimulikia na kuwamulikia wengine ili utoke gizani,umezaliwa kung`ara na si kukaa gizani.

Wengine wana taa ambazo zinapaswa kuwamulikia wengine na kwa kutokujua wamesababisha giza kwenye maisha ya watu wengi.

Ni vizuri kutumia taa yako kuwamulikia wengine usiweke taa yako chini ya kitanda maana haitakua na manufaa kwako wala kwa jamii yako.

Iweke taa yako juu ya  kinara sehemu iliyoinuka ili iweze kuwaangazia wengine kwani taa hiyo itakua na umuhimu tofauti na ile iliyowekwa uvunguni mwa kitanda.
Nikiwa Chuoni Mwalimu wangu aliniambia ukiona taa inawaka kwenye nyumba ya  jirani  usiipige mawe kwani inaweza kukuangazia na kuwaangazia wengine walioko mbali.

Nilijifunza kutowapiga vita,majungu watu wenye taa nikiamini kuwa kuna siku naweza kunufaika na taa hizo zikiwaka zinaweza kuniangazia na mimi.

Kila mtu kwenye maisha anatamani kung`ara kufanikiwa lakini tatizo hawajui kutumia kutumia mwanga ,taa walizonazo ama kuziweka mafuta ili ziweze kuangaza zaidi.

Wako ambao walishindwa kuweka taa zao mafuta zikazima,vipaji vikazima jambo ambalo ni hatari kwenye maisha ya kila siku.

Pia kuna baadhi ya watu ambao wanaamini kuwa wakizima taa za wenzao taa zao zitawaka zaidi na kuonekana jambo ambalo sai kweli,kila mtu atang`aa kwa mwanga wake (shine with your own light) .

Kila mtu amezaliwa ang`ae kila mahali alipokusudiwa  kung`aa na aliyekuumba ,iwe ni kiuchumi,kifamilia,sanaa ,filamu n.k  .

Ang`ae kwa kile alichonacho ndani yake ndicho kitamfanya ang`are mpaka kuwashangaza watu na kufurahiwa,kuwa maarufu na kufanikiwa sana kutokana na kile ulichonacho.

Inuka Uangaze

0765938008

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top