PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: BAADA YA KUSOTA POLISI SAA 175 LEMA APELEKWA MAGEREZA LEO KUSUBIRIA KESI YAKE NOV 11
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema akiwa anapanda kwenye gariya polisi mara baada ya kulazimika kwenda...

 




Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema akiwa anapanda kwenye gariya polisi mara baada ya kulazimika kwenda mahabusu katika gereza kuu la Kisongo lililopo mkoani hapa kutokana na kuwekewa na pinganizi la dhamana
Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema akiwa anapanda kwenye gariya polisi mara baada ya kulazimika kwenda mahabusu katika gereza kuu la Kisongo lililopo mkoani hapa kutokana na kuwekewa na pinganizi la dhamana
mke wa mbunge  wa jimbo la Arusha mjini Neema Lema akiwa anaondoka mahakamani  kumsindikiza mme wake mara baada ya mahakama kuisha na lema kuamriwa kwenda mahabusu ya magereza hadi ijumaa ambapo kesi yake itatajwa tena

Mbunge wa Arusha Mjini Godbles Lema ambaye alishtakiwa kwa kosa la kutoa maneno ya uchochezi dhidi ya viongozi wa serikali, leo November 8 amefikishwa mahakama ya hakimu mkazi Arusha na kusomewa shtaka linalomkabili baada ya kukaa mahabusu kwa siku saba.

Hakimu mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi anayesikiliza kesi hiyo Desdery Kamugisha amesema hawezi kutolea maamuzi kwenye mahakama hiyo kwa kuwa anahitaji muda wakusoma na kupitia vifungu vya sheria na hoja zilizotolewa na November 11 atatoa maamuzi.

Kutokana na hatua hiyo Godbless Lema amerudishwa mahabusu hadi November 11 mwaka huu. Wakili wa Chadema John Malya amesema kutokana na hoja zote zilizowasilishwa kwa pande zote mbili zimeonekana zina uzito hivyo wanasubiri uamuzi wa mahakama.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top