TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Chama Cha Mapinduzi (CCM)
kimepokea kwa majonzi na simanzi kubwa taarifa za kifo cha Mhe. Samuel John
Sitta, Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kilichotokea
usiku wa jana tarehe 6/11/2016 katika hospitali ya Technical University of
Munich nchini Ujerumani alipokuwa akitibiwa.
Mhe. Samuel John Sitta, amewahi
kushika nyadhifa mbalimbali za utumishi katika Chama na Serikali. Alikuwa
Katibu wa CCM na Mkuu wa Mkoa, Mkurugenzi Mkuu wa kituo cha uwekezaji, Mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Mjumbe wa Kamati Kuu, Mbunge, Waziri na
Spika.
Mhe. Sitta alikuwa ni
Kiongozi mchapakazi, mwadilifu na aliyejitambulisha kwa utendaji wenye kufuata
falsafa yake ya “kasi na viwango”. Ametoa mchango mkubwa katika ujenzi wa Chama
na Serikali.
Katibu Mkuu wa CCM Ndg
Abdulrahman Kinana amemtumia salamu za rambi rambi Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, familia ya Mhe. Sitta pamoja na Wananchi
wa Jimbo la Urambo kufuatia kifo cha Kiongozi huyu. Tunaungana nao katika msiba
huu ambao pia ni msiba wetu
Mwenyezi Mungu aiweke
roho ya marehemu mahali pema peponi, Ameni
Imetolewa na:-
CHRISTOPHER OLE SENDEKA (MNEC)
MSEMAJI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
07 – 11 - 2016
Post a Comment