PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: RC Mrisho Gambo apigiwa simu Rais Magufuli. Soma walichozungumza
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Mkuu wa Mkoa wa Arusha amesema kuwa Rais Dkt John Pombe Magufuli amempigia simu  na kumwambia kuwa ana imani naye na kuwa ha...


Mkuu wa Mkoa wa Arusha amesema kuwa Rais Dkt John Pombe Magufuli amempigia simu  na kumwambia kuwa ana imani naye na kuwa hajafikiria kutengua uteuzi wake labda kumpandisha cheo.

Hayo yamesemwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  baada ya taarifa kuhusu Rais kutengua uteuzi wake kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Mkuu wa mkoa alisema kuwa alipigiwa simu nyingi na watu wengi lakini kabla hajawajibu Rais Magufuli akampigia simu na kumueleza kuwa ana imani naye na kuwa ahakikishe anawatumikia wananchi wa Arusha kwani yeye sio bosi wao bali ni mtumishi wao.

Pia mkuu wa mkoa alieleza kuwa Rais amempa maagizo ya kuhakikisha anasimamia wananchi wa mkoa wa Arusha walipe kodi kwa ajili ya maendeleo ya mkoa huo na nchi kwa ujumla.

Aidha, ili kuthibitisha kuwa ni Rais Magufuli ndiye aliyempigia simu, Rais aliomba kuongea na yeyote aliyekuwa karibu ndipo mkuu wa mkoa akampa mmoja wa waliokuwa katika mkutano huo kuthibitisha kuwa ni Rais Magufuli.

AMBAPO JUZI Habari ya kutenguliwa kwa mkuu wa mkoa wa Arusha imekuja ikiwa ni siku moja baada ya kuibuka mvutano mkali kati ya mkuu huyo wa mkoa na Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kuhusu mradi wa ujenzi wa hospitali itakayotoa huduma kwa mama na mtoto mkoani humo.
 Saa chache baada ya kusambaa taarifa zilizokanushwa na Ikulu zilizodai kuwa uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo umetenguliwa, Mkuu huyo wa Mkoa ameandika ujumbe mzito unaoonekana kuwalenga mahasimu wake.

Taarifa hizo zilizothibitishwa kuwa za uongo ziliibuka siku moja baada ya tukio la kusikitisha la kuzuka ugomvi wa maneno kati ya Mkuu huyo wa Mkoa na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi kwenye hospitali ya mama na mtoto inayojengwa eneo ya Burka nje kidogo ya jiji la Arusha, mbele ya wafadhali wa mradi huo.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Gambo ameandika, “Mara nyingi ukisikia huyu ana kufa leo au kesho, huwa anaishi miaka mingi zaidi! Nazungumzia utamaduni wetu sisi Watanzania!”

Mvutano kati ya Gambo na Lema ulianza tangu Gambo alipokuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha huku kila mmoja akimtupia lawama mwenzake kwa kutofuata taratibu na protokali.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top