PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Rais Magufuli atimiza ahadi yake kwa Balozi Omben Sefue...Amteua kuwa Mwenyekiti wa Bodi Chuo cha Diplomasia
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Hatimaye Rais John Magufuli ametimiza ahadi yake kwa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue baada ya kumteua ku...


Hatimaye Rais John Magufuli ametimiza ahadi yake kwa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue baada ya kumteua kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Cha Diplomasia.

Balozi Sefue amepata uteuzi huo jana ikiwa ni miezi kumi tangu Rais Magufuli atengue uteuzi wake [kama Katibu Mkuu Kiongozi]kwa sababu ambazo hazikutajwa huku akiahidi kumpangia kazi nyingine na nafasi yake ikajazwa na Balozi John Kijazi, .

Aidha, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Waziri wa wizara hiyo, Balozi Augustine Mahiga amewateua wajumbe sita wa Bodi ya chuo hicho cha Diplomasia.

Wajumbe hao ni Balozi Begum Taj, Balozi John Haule, Juma Salum, Profesa Mohamed Bakari, Profesa Innocent Zilihona na Mathias Abias.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa uteuzi huo umeanza rasmi Oktoba 6 mwaka huu.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top