PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: TASWA FC NA TASWA SC ZATAMBA KATIKA BONANZA LA WAANDISHI WA HABARI ARUSHA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha,Kalist Lazaro akimkabidhi Kombe la ubingwa wa Bonanza la 11 nahodha wa timu ya soka ya waandishi wa Hab...
Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha,Kalist Lazaro akimkabidhi Kombe la ubingwa wa Bonanza la 11 nahodha wa timu ya soka ya waandishi wa Habari  za michezo nchini(Taswa FC),Wilbert Molandi katika fainali la Bonanza la Waandishi wa Habari mkoa wa Arusha kwenye uwanja wa General Tyre jumapili,kulia ni Mwenyekiti wa Taswa FC,Majuto Omary  na kushoto ni Mratibu wa mashindano hayo,Mussa Juma.
Nahodha wa timu ya Netiboli ya Waandishi wa Habari za Michezo nchini, Tanzania Sports Writers Association Sports Club (Taswa SC)Zuhura Abdulnoor na mchezaji mkongwe wa Timu ya soka ya waandishi wa Habari  za michezo nchini,(Taswa FC),Muhidin Sufiani(kulia)wakifurahia ushindi.
Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha,Kalist Lazaro akizungumza katika Bonanza la 11 la Waandishi wa Habari mkoa wa Arusha.
Mchezaji nguli wa timu ya soka ya waandishi wa Habari  za michezo nchini(Taswa FC),Muhidin Sufiani akichanja mbuga kupenya ngome ya timu ya Chuo cha Uandishi wa Habari Arusha(AJTC)katika mchezo wa fainali ambao Taswa FC walishinda bao 1-0.

Wachezaji wa Netiboli wa Taswa SC na Chuo cha Uandishi wa Habari Arusha(AJTC)wakichuana vikali katika bonanza hilo ambalo Taswa SC walibamiza bila huruma 30-2
Timu ya soka ya waandishi wa Habari  za michezo nchini, (Taswa FC) na netiboli ya Waandishi wa Habari za Michezo nchini, Taswa FC Tanzania Sports Writers Association Sports Club (Taswa SC) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi na waratibu wa  bonanza la 11 la Waandishi wa Habari la Arusha.




About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top