PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Tamasha la Waandishi wa habari kanda ya Kaskazini kuunguruma september 11
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Taswa queen kutoka Dare es salaam ambaoni  mabingwa watetezi wa mchezo wa netball katika bonanza hilo ambalo walijinyakilia kikombe na fed...
Image result for bonanza la wanahabari arusha
Taswa queen kutoka Dare es salaam ambaoni  mabingwa watetezi wa mchezo wa netball katika bonanza hilo ambalo walijinyakilia kikombe na fedha taslimu shilingi laki moja na nusus
Image result for bonanza la wanahabari arusha
 mwenyekiti wa Taswa Arusha Jamila Omari kulia akiwa na mgeni rasmi Juma Pinto amabaye pia ni mwenyekiti wa Taswa Taifa  katika bonanza la mwaka juzi ambapo alitoa seti za jezi kwa timu ya chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha ( AJTC) ambao walikuwa mabingwa wa mchezo wa soka
Image result for bonanza la wanahabari arusha
washiriki wakisisliza hotuba ya mgeni rasmi wa tamasha la wanahabari mwaka 2015 aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Arusha kipindi hicho Felix Ntibenda kabla ya kutoa tuzo na zawadi kwa washindi wa michezo husika 
Image result for bonanza la wanahabari arusha
moja ya press conference iliyofanyika katika hotel ya palace hotel amabapo wadhamini wakuu wa tamasha hilo kampuni ya bia nchini TBL wakielezea juu ya ushiriki wao katika tamasha hilo na zawadi walizozitoa katika  bonanza hilo
 

 

Mwandishi wetu, Arusha

Chama cha waandishi wa habari za michezo na Burudanimkoa wa Arusha (TASWA ARUSHA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Arusha Media wameandaa  tamasha la 11 la  waandishi wa habari za michezo na burudani kanda ya Kaskazini ambalo litafanyika Septemba 11 katika uwanja wa Generat Tyre.

Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu wa TASWA mkoa wa Arusha, Mussa Juma alisema zaidi ya watu 2500 wanatarajiwa kushiriki Tamasha hilo, ambapo kutakuwa na michezo ya Soka, Kuvuta kamba, Mbio za magunia ,Kukimbiza kuku na muziki kuanzia saa nne asubuhi hadi jioni.

Juma alizitaja timu ambazo zitashiriki ni TASWA FC kutoka jijini Dar es Salaam, timu ya Radio  ORS kutoka mkoa wa Manyara, timu ya Sunrise Radio, Timu ya chuo cha uandishi habari Arusha, timu ya MJ Radio na timu ya Triple a Radio.

Katika tamasha hilo, pia kutakuwa na timu za vyuo vya uandishi habari vya mkoa wa Arusha, chuo cha habari Maalum, Tasisi ya habari na mawasiliano iliyopo maji ya chai, TASWA Arusha.

“tamasha litatanguliwa na semina ya siku moja ya wanahabari mkoani Arusha juu ya masuala ya michezo, Utalii wa ndani na umuhimu wa Uwekezaji katika taifa”alisema

Mratibu wa Tamasha hilo, Andrea  Ngobole alifafanua kuwa pia kuna timu ambazo zimealikwa ambazo ni Kitambi Noma, Timu ya TANAPA,timu ya TBL Arusha, timu ya PEPSI na Coca Cola na  Wenyeji  timu ya Wazee Klabu.

Ngobole alisema Septemba 3, TASWA na Arusha Media watatangaza zawadi kwa washindi, wadhamini wote na Mgeni rasmi.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top