Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo(Katikati) akikata utepe kama ishara ya maadhimisho ya maiaka 50 ya
Utume Burka,kushoto ni Mch. Mchungaji Eliasi Ijiko na kulia ni Askofu Godwin
Godwin Lekundayo.
ARUSHA.
Viongozi wa dini nchini wameombwa kuhamasisha waumini wao kufanya kazi
kwa bidii na kulipa kodi ili kuongeza kasi ya kuleta maendeleo katika Taifa la
Tanzania na pia wametakiwa kuhamasisha waumini wao kuhakikisha wanadai
risiti kila wanapoenda kununua bidhaa au kupata huduma mbalimbali.
Kauli hiyo ilitolewa jana mjini hapa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho
Mashaka Gambo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Dr John Joseph Pombe Magufuli aliyekuwa mgeni rasmi katika
Maadhimisho ya miaka 50 ya Utume wa Kanisa la Waadventista wa Sabato.
Akizungumza na waumini na viongozi wa Kanisa hilo lililopo Burka mjini hapa,
Mkuu wa Mkoa Arusha Gambo alisema, Watanzania wanalojukumu la kufanya
kazi kwani hata Vitabu vya Dini vimeelekeza kuwa mtu asiyefanya kazi na asile
na mafundisho hayo ya dini yanaendana na falsafa ya hapa kazi tu.
Mhe. Gambo aliendelea kusisitiza kwamba kutokana na maelekezo hayo ya
vitabu vya dini ni wazi kwamba kila mtu anatakiwa kufanya kazi kwa kadiri ya
uwezo aliopewa na Muumba ili apate riziki hatua itakayowezesha pia
kupunguza wategemezi katika Taifa letu.
Akizungumza katika maadhimisho hayo RC Gambo kwa niaba ya Rais Magufuli
alisisitiza kuwa ni vyema kwa kila mmoja wetu kufanya kazi na kulipa Kodi.
"Kwa yule ambaye hatalipa Kodi ajue kwamba anaikosesha nchi yake mapato
ambayo yangeweza kutumika kuendesha shughuli mbalimbali za maendeleo, pia
tutambue kwamba huduma zote ni gharama na zinatokana na kodi tunazolipa.
Hivyo katika Serikali ya Awamu ya Tano asiyefanya kazi na asile na zaidi ya
hapo asiyelipa kodi ni vyema akafahamau kwamba analirudisha taifa lake
nyuma. Niwaombeni sana viongozi wa Dini muhamasishe waumini walipe kodi
kwa mustakabali wa Taifa letu"
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista wa Sabato
Ulimwenguni Mch. Geofrey Mbwana akitoa somo fupi wakati wa maadhimisho
hayo alisema amefurahishwa sana na uteuzi wa Mhe. Gambo na ana imani na
vijana kwa sababu vijana wakati wao ni sasa na pia ni Taifa la leo hivyo
wakipewa nafasi kama hii hudhihirisha vipawa vilivyomo ndani yao na bila
shaka Mkoa wa Arusha utakua Mkoa kielelezo kwa Taifa hili.
Kanisa hili la Sabato katika Tanzania lilianzishwa Katika kijiji cha Giti kilichopo
Mamba Miamba huko Same mnamo mwaka 1903 na kuendelea kukua katika Mji
wa Shirati Mara na kisha kufika Arusha na kuanzisha Kanisa la Burka mwaka
1966 likiwa na Jengo moja dogo na waumini nane tu.
Hivi sasa Kanisa hili lina majimbo mawili na waumini zaidi ya 500,000
Tanzania. Kanisa hili pia wanamiliko Chuo Kikuu kimoja, Shule za Sekondari 17,
Msingi 11 na shule za awali 11. Pia Kanisa hili lina Hospital moja, Kituo cha
Afya kimoja na Zahanati 28.
RC Gambo aliendelea kuwaomba viongozi mbalimbali wa dini wazidi
kumuombea na kumtia Moyo Mhe. Rais katika kazi yake ngumu na kubwa
anayoifanya kwa maslahi ya Taifa haswa kusaidia wanyonge ambao kwa muda
mrefu hawakuwa sehemu ya Agenda kubwa ya Serikali. Pia waendelee
kuwasisitiza wanasiasa watambue kuwa wakati wa Siasa umekwisha ni vyema
Mhe. Rais akapewa nafasi ya kuwatumikia watanzania kwa yale aliyoyaahidi
kupitia utekelezaji wa ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI na watakutana tena
kwenye siasa mwaka 2019 - 2020.Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho
hotuba ya Mgeni Rasmi kwa viongozi wa kanisa na waumini wa Kanisa la
Waadventista wa Sabato.
Katika picha ya pamoja ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo
(katikati) na viongozi wa Kanisa la Waadventista wa Sabato.
Mchungaji Eliasi Ijiko akimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho
Gambo vitabu na majarida mbalimbali yanayochapishwa na Taasisi za kanisa la
wasabato Tanzania
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(Kushoto) akiendelea
kutembelea mabanda ya maonyesho katika maadhimsho ya miaka 50 ya Kanisa
la Wasabato, Burka.
Post a Comment