NA: ISMON MJEMA, SAME:
Serikali Wilayani Same imeagiza kupewa nakala ya vikao vyote
vya Serikali Wilayani hapo,kuanzia ngazi
ya Kijiji, Kata (WODC) hadi Halmashauri ili kufuatilia kwa ukaribu utekelezwaji wa agizo la kufanya
vikao vya kisheria,ikiwemo ufuatiliaji wa utekelezaji wa Muhtasari wa vikao
husika.
Akizungumza na Baraza la Wazee Kata ya Suji,mara baada ya
kumaliza kushiriki katika Msaragambo wa ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha
Malindi na Kituo cha Afya cha Kata hiyo,Mkuu wa Wilaya ya Same,Rosemary Staki
Senyamule,nakala zote za vikao vya Serikali zinazopelekwa kwa Mkurugenzi wa
Halmashauri,zipelekwe Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ili Ofisi hiyo iweze kufuatilia
vikao hivyo kwa ukaribu zaidi;Ikiwemo kuona Tija inayotokana na Vikao hivyo.(
201 609 053 15 16-DC)
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wazee Kata ya Suji wameusifu
uamuzi wa Mkuu huyo wa Wilaya,kwa kutaka nakala za vikao Serikali vya kisheria
kwa kudai kuwa itaongeza ufanisi wa utekelezaji wa maazimio ya vikao.
Vijiji kadhaa nchini, Serikali za Vijiji hivyo zimekuwa
zikituhumiwa kutokusoma mapato na matumizi na kutokufanya vikao halali vya
kisheria na wananchi,hali ambayo imekuwa ikiwaacha wananchi njia panda wakiwa
na maswali yasiyo na majibu na kupelekea Watu kutokuwa na Imani na Viongozi
wao.
Post a Comment