ZAHANATI ya Selela iliyopo wilayani Monduli mkoani Arusha. Picha na Ferdinand Shayo
Ferdinand Shayo,Arusha.
Wajawazito
katika zahanati ya kijiji cha Selela kata ya Selela wilaya ya Monduli mkoani Arusha
wamelazimika kujifungua kwa kutumia tochi za simu pamoja na taa ya chemli
kutokana na kukosekana kwa huduma ya umeme kwa takribani mwezi mmoja na wiki
mbili.
Kinamama wa
kijiji hicho tumaini shirima na mwasiti hemedy
wameeleza kuwa wamekua wakiwapeleka wajawazito kwenye zahanati hiyo kwa
ajili ya kujifungua na kushuhudia wauguzi wakitumia tochi za simu kutoa huduma
kwa wajawazito jambo ambalo linawafedhesha hivyo wameiomba serikali isaidie
upatikanaji wa huduma ya nishati ya umeme ili waweze kupata huduma bora.
“Tunapata
shida hata tunapowapeleka Wajawazito zahanati hakuna umeme wauguzi wanatumia
tochi za simu ,juzi tulimpeleka mwenzetu akajifungue tuliona hilo likijitokeza
kwa sababu umeme hakuna”
Mganga wa
zahanati hiyo Michael Msalu alisema kuwa nyakati za usiku wanalazimika kutumia tochi
jambo ambalo linaweza kuathiri afya ya mama mjamzito na mtoto ,vile vile
wameshindwa kufanya baadhi ya vipimo maabara kutokana na kukosa huduma ya umeme
.]
Msalu
anaeleza kuwa si jambo zuri kiafya kushika simu huku unamhudumia mama mjamzito
unaweza kusababisha maambukizi kwani huduma hiyo inahitaji uangalifu mkubwa ili
kulinda afya ya mama na mtoto pamoja na mtoa huduma.
Diwani wa
kata ya Selela Cathbet Meena amesema kuwa licha ya zahanati hiyo shughuli za
kiuchumi na kijamii zimesimama katika kata hiyo ikiwemo biashara,mashine za
kusaga nafaka kwa muda wa mwezi mmoja na wiki mbili baada ya transfoma
iliyowekwa na Tanesco kupata hitilafu baada ya kuwasiliana na mamlaka hiyo
imekua ikitupiana mpira kati ya Rea
katika maboresho hayo.
Kwa upande
wake Kaimu Meneja wa Mkoa wa Arusha
Tanesco ambaye ni Mhandisi Mkuu Donasian Shamba amekiri kuwepo kwa
tatizo hilo ambalo linasababishwa na masuala ya kitaalamu yanayopelelekea transfoma
kuungua mara kwa mara hivyo wametuma timu ya wataalamu na mapema wiki hii
watarekebisha tatizo hilo ili wananchi wapate huduma.
wakazi wa
selela wamelazimika kusimamisha shughuli zao za uchumi zinazotegemea nishati ya
umeme hivyo wanaiomba serikali ichukue hatua ili waweze kurudi katika shughuli
za uzalishaji zinazowaingizia kipato.
|
Post a Comment