PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Polisi Wamnyima Tundu Lissu Dhamana, Atupwa Rumande
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
JESHI la Polisi, kanda Maalumu ya Dar es Salaam limemnyima dhamana, Tundu Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo ...
JESHI la Polisi, kanda Maalumu ya Dar es Salaam limemnyima dhamana, Tundu Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), baada ya kumaliza kuhojiwa katika kituo kikuu cha polisi.

Baadhi ya viongozi waliofika kumwekea dhamana  ni pamoja na  Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Chadema, Edward Lowassa Waziri Mkuu wa zamani na mjumbe wa kamati kuu wa Chama hicho, aliyefika saa 12:14 jioni akiungana na viongozi na wanachama wa chama hicho.

Baada ya kufika Lowassa wanachama na wafuasi wa Chadema waliokuwa nje ya ofisi hizo za polisi walianza kuimba wimbo wa kumuita rais, rais, rais ikiwemo na kauli mbiu ya maarufu ya Peoles power.

Mara baada ya kufika alipokelewa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe aliyekuwa amepanda gari moja na Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob waliokuwa nje ya geti.

Viongozi hao waliokuwa nje baada ya kuzuiwa kuingia ndani na polisi waliongozana na Lowassa kuomba kuingia lakini walizuiwa hali iliyofanya wachukue uamuzi wa kuondoka.

Kiongozi aliyeruhusiwa kuingia alikuwa ni Meya wa Dar es Salaam, Isaya Mwita.

Akizungumzia kuhusu hilo, Peter Kibatala mwanasheria wa Lissu alisema kwamba mahojiano kati ya jeshi hilo na mtuhumiwa yalianza saa 9:30 hadi saa 12:30.

“Katika maelezo ya polisi wanasema kwamba wakati Lissu akitoka mahakamani juzi kwenye kesi yake  alitamka maneno ya uchochezi, lakini haya yote yanahitaji ushahidi,” alisema Kibatala.

Wakili huyo alisema kwamba polisi baada ya kumaliza mahojiano na wao wakiwa wameandaa utaratibu wa dhamana walikataliwa hadi leo Ijumaa atakapofikishwa mahakamani.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top