Mkuu wa TV 1, Joseph Sayi (katikati),akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam kuhusu Kituo cha
Televisheni cha TV1 Tanzania kuanza kurusha matangazo ya moja kwa moja
ya mpira wa miguu ya ligi kuu soka ya Uingereza EPL matangazo ambayo
yanatarajia kurushwa kuanzia Agosti 13 mwaka huu. Kulia ni Meneja Masoko wa TV 1, Gillian Rugumamu na Meneja Masoko Startimes, kushoto ni Felix Awino
Meneja Masoko wa TV 1, Gillian Rugumamu
(katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es
Salaam leo kuhusu Kituo cha Televisheni cha TV1 Tanzania kuanza kurusha
matangazo ya moja kwa moja ya mpira wa miguu ya ligi kuu soka ya
Uingereza EPL matangazo ambayo yanatarajia kurushwa kuanzia Agosti 13
mwaka huu. Kushoto ni Mkuu wa TV 1, Joseph Sayi na kulia ni Mchambuzi wa
Michezo Dk. Leakey Abdallah.
Mchambuzi wa Michezo Dk. Leakey Abdallah (katikati), akizungumzia masuala ya mpira katika mkutano huo.
Production Meneja wa TV 1, Mukhsin Khalfan Mambo akizungumza katika mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Wanahabari wakiwa kazini.
Taswira ya meza kuu katika mkutano huo.
Mchambuzi wa michezo, Ally Kashushu (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
Mmiliki wa Blog ya Kajuna Son, Cathibert Kajuna (kulia), akiuliza swali katika mkutano huo.
Baadhi ya wafanyakazi wa TV 1 wakiwa wakifuatilia matukio mbalimbali ya mkutano.
Na Dotto Mwaibale
KITUO cha Televisheni cha TV1 Tanzania
kinatarajia kuanza kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mpira wa miguu
ya ligi kuu soka ya Uingereza EPL matangazo ambayo yanatarajia kurushwa
kuanzia Agosti 13 mwaka huu.
Ligi kuu soka nchini Uingereza ndio ligi
maarufu zaidi duniani na hii ni kutokana na kushirikisha timu kongwe
zenye ubora na mashabiki dunia nzima ikiundwa na timu maarufu duniani
kama vile Manchester United,Liverpool, Arsenal pamoja na Chelsea.
TV1 Tanzania ndio kitakuwa kituo pekee
cha runinga hapa nchini kupewa haki za kurusha matangazo haya
yatakayokujia moja kwa moja yaani Live yakihusisha pia uchambuzi wa ligi
hiyo ambapo kutakuwa na vipindi vya kabla ya mechi na baada ya mechi
husika.
Kwa upande Mkuu wa Kituo cha TV 1
Tanzania Joseph Sayi alisema hii ni fursa kubwa kwa wadau wa soka hapa
nchini kuishuhudia ligi hiyo moja kwa moja, Mkuu wa kitengo cha masoko
wa TV1 Gillian Rugumamu alisema lengo ni kuwapelekea watazamaji wao wa
Tanzania ligi kuu England ambayo ni ligi inayopendwa na kufuatiliwa na
Watanzania.
Baadhi ya watangazaji na wachambuzi
watakaokuwa wakishiriki katika urushaji wa matangazo hayo na uchambuzi
ni Ally Kashushu na Dkt. Leakey Abdallah ambaye ni mchambuzi mwenye
uzoefu wa miaka 20 kwenye tasnia ya michezo husasani uchambuzi.
Mchambuzi wa Michezo Dk. Leakey alisema
watanzania wategemee uhondo wa ligi hiyo kutokana na uwepo wa wachezaji
nyota na makocha mahiri kama Antonio Conte,Arsene Wenger,Jurgen Klopp na
makocha hasimu Jose Mourinho wa Manchester United na Pep Guardiola wa
Manchester City.
Tv1 Tanzania ni kituo cha runinga
kilianza mwaka 2013 ambapo kilianza kurusha matangazo yake rasmi
Januari 2014 ambapo kimekuwa kikiandaa na kurushwa vipindi vyenye ubora
wa hali ya juu ambapo TV 1 inapatikana kupitia ving’amuzi vya Startimes
namba 103,Azam 119 na Ting 36.
Post a Comment