PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MANJI: MURO BADO YU MFANYAKAZI HALALI WA YANGA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
MWENYEKITI wa Yanga, Yusuf Manji, amevunja ukimya na kusema Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Jerry Muro yupo hur...
MWENYEKITI wa Yanga, Yusuf Manji, amevunja ukimya na kusema Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Jerry Muro yupo huru na anaendelea na kazi zote za klabu kama kawaida.
Manji ameliambia Championi Jumatatu kwamba, klabu hiyo haina taarifa yoyote rasmi ya kufungiwa kwa Muro.
“Kama taarifa tumesikia kwenye magazeti na redio, kweli taasisi kama Yanga, msemaji wake anasimamishwa kwa njia hiyo?
“Hao waliomsimamisha pia ni taasisi, vipi wafanye hivyo. Yanga tunawezaje kuamini hilo? Muro bado yuko kazini na anaendelea na shughuli zake kama kawaida,” alisema Manji.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top