Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla,akitolea ufafanuzi na kujibu kero
mbalimbali zilizotolewa na wananchi wa Mkoa wa Mbeya, katika kikao
maalum cha kupokea kero za wananchi kilichofanyika kwenye ukumbi wa
mikutano wa Mkapa, ambapo kubwa zaidi katika siku hii, Makala amesema
serikali itahakikisha inamkamata mkandarasi wa ujenzi wa uwanja wa ndege
wa Songwe kutoka kampuni ya Kundan Sigh, baada ya kushindwa kulipa
mafao ya vibarua zaidi ya 50.
|
Na EmanuelMadafa,Mbeya
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos
Makalla ameagiza kukamatwa kwa mmiliki
wa kampuni ya Kundan Singh, ambaye alipewa tenda ya kujenga uwanja wa ndege wa
Songwe, baada ya kushindwa kulipa mafao
ya vibarua zaidi ya 50.
Mkuu huyo wa Mkoa wa
Mbeya ametoa kauli hiyo , wakati akijibu na kutatua kero mbalimbali za wananchi
ambazo hazijapatiwa ufumbuzi kwa kipindi kirefu, hali iliyochangia wananchi
kuichukia serikali kwa madai ya kushindwa kuwatendea haki.
Awali, akitoa
malalamiko hayo kwa Mkuu wa Mkoa, Joshua Mwasilonde kwa niaba ya vibarua
wenzake, amesema wamekuwa wakidai mafao yao tangu mwaka 2012/2013 katika mfuko
wa hifadhi ya jamii NSSF na kwamba kila wanapofuatilia wamekuwa wakipigwa
kalenda.
Akilizungumzia hilo,
Makala amesema, kwakua serikali iliingia mkataba na kampuni hiyo na kumalizana
nayo bila ya kuacha deni lolote hivyo mkandarasi huyo anapaswa kuwalipa vibarua
hao na kuutaka uongozi wa NSSF, kuhakikisha unavishirikisha vyombo vya dola
katika kumkamata mkandarasi huyo.
Meneja NSSF Kanda ya
Nyanda za Juu kusini, Robert Kadege, akilitolea ufafanuzi suala hilo, amesema
suala la vibarua hao linafanyiwa kazi na kwamba tayari mahakama imetoa hukumu
na kuupa ushindi mfuko huo..
Mwisho.
Katibu tawala Mkoa wa Mbeya Mariam Mtunguja, akitolea ufafanuzi baadhi ya masuala ya kiutendaji katika kikao hicho.
|
Baadhi ya wananchi waliofika kutoa kero na malalamiko katika kikao hicho.
|
Baadhi ya viongozi na watendaji wa serikali katika kikao maalum cha kupokea kero za wananchi kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Mkapa June 29 mwaka huu.
|
Baadhi
ya wananchi wakitoa malalamiko na kero zao katika kikao maalum cha
kupokea kero za wananchi kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa
Mkapa June 29 -2016 ambapo MKuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ndiye
aliyepokea kero hizo sanjali na watendaji wa serikali na taasisi
mbalimbali za serikali .
|
Kikao kikiendelea.(Picha E.Madafa)
|
Post a Comment