Kutokana na hatua hiyo, hoteli maarufu zilizopo Dar es salaam pamoja na mikoa mingine zimelazimika kufungwa na huku nyingine zikibadilishwa na kuwa hosteli kwa ajili ya kuhudumia wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu na kati.
Mbali na hilo pia baadhi ya wamiliki wa hoteli hizo wamelazimika kupunguza wafanyakazi kama njia ya kukabiliana na athari za ukosefu wa mapato.
Baada ya kuapishwa na kuingia madarakani Novemba 5 mwaka jana Rais Magufuli alitangaza hatua kadhaa za kubana matumizi yasiyo ya lazima ikiwamo kuwataka watendaji wa mashirika ya umma kutofanya mikutano katika kumbi za mahoteli na ikiwezekana wafanyie chini ya miti.
Uchunguzi uliofanywa na mtanzania kwa wiki mbili sasa umegundua kufungwa kwa hoteli maarufu jijini Dar es salaam na nyingine mkoani Pwani, hoteli ambazo zimefungwa kutokana na sekeseke hilo ni Land mark hotel iliypo ubungo Dar es ambayo kuanzia September mosi itaanza kutoa huduma za hosteli.
Kwa upande wa hoteli ya Jb Belmont zilizopo katika majengo ya Benjamini Mkapa na Golden Jubilee jijini Dar es salaam nazo zimefungwa huku walinzi wakibaki kuzunguka katika maeneo hayo kulinda mali.
Post a Comment