PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MAKALA YA UCHUMI: KIPAJI CHAKO NI ZAIDI YA FEDHA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Na Ferdinand Shayo,Arusha. Watu wengi duniani wametajirika kutokana na vipaji walivyonavyo   wakiwemo Wanamuziki,Waigizaji,Wachora...
https://scontent.xx.fbcdn.net/v/t1.0-1/p160x160/13346822_1200798256606625_4369056893226362969_n.jpg?oh=b657d56559ebbce1081146b8691d4954&oe=57F331D3

Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Watu wengi duniani wametajirika kutokana na vipaji walivyonavyo  wakiwemo Wanamuziki,Waigizaji,Wachoraji ,Wabunifu ,Wagunduzi na Wavumbuzi wa mambo mbalimbali.

Watu waliogundua uwezo walionao ,upekee na umaalumu na kuutumia kwa manufaa yao nay a jamii yao ndo waliofanikiwa zaidi kwenye ulimwengu wa leo.

Vipaji walivyonavyo vimegeuka kuwa mashine ya kuzalishia fedha na kuwapa kuishi maisha wanayoyataka.

Ukifanya uchaguzi utagundua  kuwa watu wenye vipaji wanalipwa vizuri kuliko watu walioajiriwa .

Kipaji hakizeeki wala kustaafu ,Leo hii Wanamuziki kama King Kiki,Msondo ngoma bado wanafanya muziki na kujiingizia kipato wangekua wameajiriwa serikalini tayari wameshavuka muda wa kustaafu wangekua wako nmajumbani wanakula pensheni  na wengine kuugulia ugumu wa maisha.

Kipaji kinaweza kukupa maisha unayoyataka tofauti na kazi ya kuajiriwa inakulazimu kuishi maisha kulingana na mshahara unaoupata.

Ndugu yangu usidharau kipaji ulichonacho kwani ni kitu cha thamani sana na cha pekee na cha tofauti ambacho si kila mtu anacho isipokua wewe.

Kila mtu duniani ana kipaji ama uwezo Fulani wa  kipekee na maalumu .Hakuna mtu aliyeumbwa kama kasha tupu lisilo na kitu .

Una kitu cha thamani ndani yako jiamini,jikubali,jiongeze kwa kuchukua hatua kutumia kipaji ulichonacho kubadilisha maisha yako.

Kipaji kinapaswa kukuzwa kama mche wa mti kwa kumwagiwa maji,mbolea na kupata mwanga ili kiweze kukua ,kustawi na kuzaa matunda ,matunda ambayo ni mafanikio,fedha,umaarufu,utajiri na vingine vingi.

Lazima kuwe na mazingira bora ya kuvumbua na kukuza vipaji kuanzia kwa watoto wadogo,vijana na hata wazee vipaji vyao vinaweza kuwa rasiliamali muhimu na tunu kwa taifa.

Kutengeneza mazingira rafiki yanayoruhusu vipaji vya watu kujitokeza na kuonekana nje  mithili ya kuku anayetaka kutaga lakini ni juu yam awe anaweza kutaga yai likapasuka.

Tengeneza Mazingira bora ya kugundua ,kukuza na kuendeleza vipaji kwa faida ya jamii,taifa na dunia kwa ujumla.


0765938008

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top