Uuzwaji wa nyumba za serikali umegeuka mwiba huku wabunge wakiendelea kuhoji hatua zilizochukuliwa kutokana na kadhia hiyo
Hatua hiyo iliyotekelezwa mwaka 2002 hadi 2004 ilizusha malalamiko mengi tangu wakati huo na sasa imeibuka tena bungeni
Akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
mawasiliano jana, mbunge wa Nachingwea, Hassani Masala (CCM) alihoji
mfumo uliotumika kuuza nyumba za serikali
Alisema haungi mkono kwa vile umesababisha viongozi wapya wa serikali wanaoteuliwa kujikuta wakiishi katika nyumba za wageni.
Mjadala huo uliibuliwa juzi na msemaji wa kambi ya upinzani Bungeni
kupitia kwa waziri kivuli wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Godbless
Lema kabla ya Mwenyekiti wa Bunge Mussa Azzan Zungu kumtaka kuondoa
baadhi ya maneno katika hotuba yake likiweo suala la uuzwaji wa nyumba
za serikali.
Ritha Kabati Amvaa Lowassa
Akichangia mjadala huo jana, Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Ritha Kabati
alimtaja aliyekuwa mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), Edward Lowassa kuwa alinunua nyumba ya serikali iliyouzwa
mwaka 2002 yenye jengo namba 68.
Alisema hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ilisema nyumba za
serikali 7,921 ziliuzwa tangu mwaka 2002 hadi 2004 na kutaka serikali ya
awamu ya tano kurejesha nyumba hizo kutokana na walionunua kukiuka
mikataba na malengo ya mauzo.
“Naomba niwaambie usiangalie boriti lililo katika jicho la mwenzako
wakati kwako lipo, kwani hata mgombea wao wa urais Edward Lowassa
alihusika kwa kununua nyumba ya plot namba 68 na Fredrick Sumaye alikuwa
Waziri Mkuu na kuhusika kuuza nyumba hizo,” alisema Kabati.
Baada ya kueleza hayo, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na
Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe (Chadema) aliomba kumpa taarifa mbunge huyo
kuwa taarifa hiyo ni kwa maslahi ya taifa, hata kama mhusika atakuwa
katokea kambi ya upinzani sheria itachukua hatua.
"Kambi ya upinzani tunapoibua jambo huwa linakuwa kwa maslahi ya Taifa,
hivyo ni vyema wabunge wote mtambue kuwa kosa likifanywa na kiongozi ni
lazima hatua zichukuliwe bila kujali ni wa Chadema, CUF au CCM.
"Tunapokuwa tunatoa uamuzi kama kambi ina maana sheria ifuate mkondo wake." Alisema Mbowe huku akishangiliwa na wabunge wa UKAWA
Awali katika michango mbalimbali ya wabunge wa upinzani wamekuwa
wakilalamikia kuuzwa nyumba hizo za serikali na kudai kuwa watumishi
wapya wengi walioajiriwa, wamekuwa wakikosa maeneo ya kuishi.
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) akichangia mjadala huo
alilalamikia kuuzwa kwa nyumba hizo pamoja na nyingine za Tazara
zipatazo 500 na kuamua kumpatia Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na
Mawasiliano ripoti aliyodai inaonesha nyumba hizo zilivyouzwa.
Home
»
HABARI ZA BUNGE
» Lowassa na Sumaye Watajwa Katika Sakata la Uuzwaji wa Nyumba za Serikali.......Mbowe Atoa Ufafanuzi
About Author
Journalist , Enterpreneur, Lecturer and Blogger. Email :ngoboleaa@gmail.com.
Advertisement
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment