Adhabu hiyo iliyotolewa jana jioni bungeni mjini Dodoma inamaanisha kuwa wabunge hao hawataingia bungeni hadi mwaka 2017.
“Mimi na Halima tunasimamishwa shughuli za bunge mpaka mwezi Septemba,” alitweet Zitto ambaye ni mbunge wa Kigoma Mjini.
“Wabunge wote wa upinzani wamepewa onyo kali kwa kung’ang’ania kutaka bunge lioneshwe moja kwa moja na shirika la TBC.”
Wabunge wengine waliopewa adhabu na kamati ya maadili, haki na madaraka ya bunge ni Pauline Gekuli na Godbless Lema ambao hawatahudhuria vikao vyote vya mkutano wa tatu.
Mbunge John Heche amepewa adhabu ya kutoshiriki vikao 10 vya mkutano wa tatu.
Post a Comment