PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: DEGREE/DIPLOMA SIO KAZI SEHEMU YA TANO
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  NA ADSON KAGIYE KAZI NI KUIFANYIA KAZI HIYO DEGREE/DIPLOMA Lazima uwe na jambo unalolisimamia katika maisha na jambo len...

 
https://lh6.googleusercontent.com/-xIpjgqv2UcA/AAAAAAAAAAI/AAAAAAAAAAA/F_1A0MyWG1s/s128-c-k/photo.jpg
NA ADSON KAGIYE

KAZI NI KUIFANYIA KAZI HIYO DEGREE/DIPLOMA

Lazima uwe na jambo unalolisimamia katika maisha na jambo lenyewe liwe la kijamii. Wengine hukata tamaa na kuanza kufikiria ningekuwa kama yule basi ningekuwa vile na vile unasahau ya kwamba hapo ulipo umekalia madini. ZAMANI KIDOGO MIAKA YA 90 MWINYI ALIWAHI KUSEMA WANAWAKE MMEKALIA UTAJIRI - ingawa alitafsiriwa vibaya, ukweli ni kwamba wanawake wa Taifa hili ndio wanalisha taifa hili kwa kuwa kila siku wanaamka asubuhi na kwenda mashambani na kuzalisha chakula takribani 70% tunachokula. kama watageuza na kuongeza ziada kwa ajili ya biashara basi huo ndio utajiri waliokalia.
Unaweza kuwa unasikitika sna kwamba kozi (course) hii haiajiriki au hainaga ajira au haina kazi yaani ukimaliza unasubiria tu serikali itoa ajira, unachosahau ni kwamba kila course ambayo ipo chuo ina FURSA NYINGI SANA shida yako fursa hizo huzioni na hujajiandaa kuziona. Siku hizi utashangaa kuona  engineer amekuwa mhasibu, lawyer amkeuwa mhuasibu, mhasibu amekuwa daktari, socilogia amekuwa mchungaji, amekuwa mwalimu, amekuwa podcaster, amekuwa mtaalamu ktk Facebook na kadhalika. 
Ndio mana tunasema sehemu nzuri kabisa ya kuanzia ni kuangalia nini wewe unakipenda, mimi ni mwalimu lakini napenda sana mambo ya kilimo, afya na biashara, ukinikuta class napiga chaki zangu vizuri sana, ukinikuta mtaani au tuseme facebook unaweza dhania umekutana na daktari mkuu. Simple napenda sana biology, na chemistry. Lakni nimeendelea kusoma vitabu vingi vya biology na kujiunga katika international journals, kujiunga ktk kampuni mbalimbali za afya na pia kujifunza mambo mbalimbali ya upishi na nutrition. Katika maeneo hayo nimeona fursa nyingi sana na zingine nikazichukua
Jifunze sana kile kitu ulicho nacho na jifunze sana kuhusu kile kitu unachokipenda. Mfano wewe umesoma journalism kwa nini usijifunze mambo mengi ya kisheria? Unamjua LISSU? unajua kilichomtoa?, yeye alikuwa mwalimu lakini alijiunga chuo akiwa na lengo moja tu kuwatetea wachimbaji wadogowadogo wanaodhulumiwa na serikali. Baada ya kuandika sana mitandaoni TV moja wakamchukua na kuanza kumrusha live (huo ni mkataba na huenda alipata pesa nyingi sna) angesubiria ajira leo hii usingemwona BUNGENI
UNAMFAHAMU - Rusigwa herbal Clinic, sio dakatari ni BA holder lakini kwa sasa ni gwiji wa mitishamba na amepata degree ya pili ya Health Management, anatafuta ya 3 ya Madawa ya Kienyeji, he mean it. Nawafahamu madkari wengi tu amabo ni MA IT, na wengi ambao ni MA MC na MA DJ- LIFE IS FULL OF OPTIONS WHAT MATTERS IS WHAT YOU LOVE AND THE KNOWLEDGE YOU HAVE
UMEKALIA UTAJIRI, UMEKIZIMA KIPAJI CHAKO. Kile unachokipenda kifuatilie mpaka mwisho, kama ulipenda jambo fulani na kwa bahati mbaya hukulisomea basi jifunze kile kinachowezekana na kukifanyia kazi. Sio lazima usome bcom ndio uwe mjasiriamali. Jifunze kuendeleza degree/diploma yako hata kama bado huna ajira, milango itafunguka kama wewe nawe utafunguka - Ifanyie kazi degree/diploma yako, haijalishi upo shule au umemaliza shule
Na .Adson kagiye

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top