MKUU WA MKOA WA DARESALAAM, PAUL MAKONDA AKIMUANGALIA ESPEDITO JACKSON BAADA YA KUMKABIDHI FUNGUO TAYARI KWA MATUMIZI YAKE. |
ROSE ANTONY AKIWA KATIKA MCHUANO MKALI WA SHINDANO LA SHIKA NDINGA, MWISHOWE ALIIBUKA MSHINDI NA KUCHUKUA GARI HIYO ALIYOISHIKA. |
MENEJA MKUU WA EFM RADIO (WA KWANZA KUSHOTO)AKIMSIKILIZA MKUU WA MKOA WA DARESALAAAM WAKATI ALIPOKUWA ANAZUNGUMZA NA WAAKAZI WA DARESALAAM KATIKA SHINDANO HILO |
SEHEMU YA UMMA ULIOHUDHULIA KATIKA TAMATI YA SHINDANO LA SHIKA NDINGA WAKISHUHUDIA USHINDANI ULIOPO |
MAKONDA AKIWAPONGEZA WALIOZAWADIWA PIKIPIKI |
Hatimaye SHINDANO la shika ndinga lililokuwa likiendeshwa na kituo cha EFM radio limefika tamati huku likishuhudia Rose Antony(23) Mkazi wa Kibaha na Espedito Jackson (Kibaha)wakiibuka washindi wa shindano hilo na kila mmoja kujinyakulia gari aina ya Suzuki zote zikiwa na thamani ya shilingi Milioni 20.
Akizungumza na fullhabari blog Meneja Mkuu wa Efm Radio Bw. Denis Ssebo amesema Kituo chake kilianzisha shindano hilo kwa dhamira ya kuinua uchumi wa wasikilizaji wake na kwamba zawadi ambazo wamezitoa zitachangia kuinua uchumi wa washindi hao
Ssebo Ameongeza kusema mbali na kutoa magari hayo pia wameweza kutoa pikipiki 2 aina ya Boxer kwa washindi wawili wa kila wilaya ambazo zimeshiriki katika shindano hilo.
Ametaja Wilaya ambazo zimeshiriki katika shindano hilo kuwa ni pamoja na Wilaya ya Kinondoni, Temeke, Ilala, Bagamoyo na Wilaya ya Kibaha ambazo kwa pamoja wamechukua jumla ya pikipiki 10 zenye Thamani ya Shilingi Milioni 20.
“Leo tuna furaha tumekamilisha shindano hili na washindi wameonekana, tunaamini zawadi ambazo tumewapatia leo zitasaidia kuinua uchumi wao… hilo ni jambo zuri kwetu kwani wasikilizaji wetu hawasikilizi bure wanasikiliza na pia wanafaidika”Aliongeza Ssebo
MKUU WA MKOA APONGEZA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amepongeza jitihada zinazofanywa na kituo cha Efm na kusema shindano hilo litachangia sehemu ya uchumi wanchi.
Alisema washindi kama watatumia zawadi hizo vizuri kujiingizia Kipato watakuwa wamejiari wenyewe na Hivyo kuisadia serikali katika suala zima la Ajira.
Amesema Biashara ya usafiri kwa sasa ni kubwa na inaingiza fedha nyingi hivyo vijana ambao wamepata gari na wale wenye pikipiki wanaweza kujikwamua kiuchumi na mwishowe kumiliki Biashara kubwa ya usafiri hapa nchini.
“Leo mmepewa zawadi hizi za Magali na mapikipiki watu wataanza kuwaganda kwa sababu mna gari…ninachotaka kuwaambia achaneni na watu wanaowaganda badala yake jipangeni kutumia vyombo hivi vya moto kuwaletea Kipato” Alisema Makonda
WASHINDI WATOA YA MOYONI
Katika hatua nyingine, mmoja wa washindi hao ambaye amejinyakulia zawadi ya juu kabisa ya gari Ms Rose Antony amesema amefarijika sana baada ya kufanikiwa kupata zawadi hiyo na kwamba ataitumia kuhakikisha inamletaea Faida.
Amesema shindano lilikuwa la wazi na halikuwa lenye upendeleo wowote toka limeanza na kwamba siri ya ushindi wake ni mazoezi ambayo alikuwa akiyafanya usiku.
“Kuolewa hapana bado sijaolewa… hiyo haimaniishi kuwa sitafanya biashara… nitahakikisha biashara hii inakuwa kubwa na inanikwamua kiuchumi ” Alisema
Akizungumzia ushindani Ms Rose alisema ushindani ulikuwa mkubwa hasa katika fainali kwani mpinzani wake alimpa wakati mgumu muda wote.
“Wakati niko kibaha nilisha nafasi ya tatu lakini nikajua wazi kuwa mimi naweza na nikaamua kufanya mazoezi ya nguvu jambo ambalo limenisaidia kushinda mpambano huu” Alisema
Hata hivyo wadau ambao waliwasili katika shindano hilo la shika Ndinga Lililofanyika viwanja vya TP Sinza, hawakusita kuwapongeza waandaji wa shindano hilo na kusema limekuwa la uwazi na haki
Wamesema wameshuhudia mshindi amepatikana hadharani pasipo kuwa na dalili za kuwabeba baadhi ya watu kitu ambacho kimewatia faraja.
Hamisi Abdallah ni mmoja wa watu waliohudhuria shindano hilo, amesema ni shindano ambalo linahitaji kupewa pongezi.
Amesema namna ya watu walivyoshiriki na hatimaye anapatikana mshindi imekuwa ya wazi na huru.
Amesema dhamira ya shindano la shika ndinga ni kuwawezesha kiuchumi wasikilizaji wa EFM na kwamba sasa ni kazi ya washindi kutumia magari hiyo vizuri ili yaweze kuwaletea maendeleo.
Post a Comment