PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: DEGREE/DIPLOMA SIO KAZI SEHEMU YA SABA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Degree manayake advanced logical thinking, at the highest level. Maana yake ni kwamba kuna baadhi ya watu hawana degree/diploma za...



Degree manayake advanced logical thinking, at the highest level. Maana yake ni kwamba kuna baadhi ya watu hawana degree/diploma za vyeti lakini wapo au wameshapitia ktk fikra za juu kabisa za mawazo na ubunifu. Hawa ni vijana wengi waliopo mtaani waliotia bidii ktk kazi zao za mikono, kijamii na kisiasa na kuweza kuleta mabadiliko makubwa ktk jamii na mabadiliko haya yanayoonekana.
Ndio mana vyuo vikuu huwa wanawapatia nishani au degree za heshima. Imagine mtu aliyegundua Microsoft hakumaliza degree na hana degree, sasa utasemaje hana fikra za juu?
Vijana wapo mitaani wamegundua mambo kadha wa kadha katika kilimo, afya na ufundi.
Mtu kama Kakobe, Mchungaji Lwakatare, hawa ni watu hata kama wanatoa mafundisho ya dini, wameweza kuunda taasisi kubwa za kiimani na kuzisimamia na kuziendeleza, swali wanadegree ngapi? Waziri mkuu wa zamani wa Tanzania (KAWAWA) hakuwa na degree wala diploma. LAKINI AMELIFANYIA MAKUBWA TAIFA HILI. By the way wakati wa vita vya Kagera alikuwa Waziri wa Ulinzi.
Ndio mana nasema kupata degree/diploma si kazi, kazi kuifanyia kazi hiyo degree.
Jana tuliona vitu vingi sana muhimu unavyotakiwa kuvijua ili kuweza kuzichakata vizuri raslimali zilizopo duniani. Na najua wengine wanaona ni kitu cha kawaida tu, wengine wanapuuzia na wengine wamekizingatia na kukifanyia kazi.
Kwa sasa huwezi kuwa na visingizio kwa nini umeshindwa kujifunza vitu. Kwa kuwa elimu hiyo ipo bure kabisa kila mahali
Googel, YouTube na Facebook ni Chuo tosha. Kuna lecture huko hadi za masaa24. Kuna Google maps, presentation nakadhalika. Sh500 tu unajifunza kitu mpaka unachoka na kuanza kusinzia.
Simu yako ni Jembe lako, hakikisha unatumia MB zako vizuri jifunze kitu YouTube, Google na Facebook. Utakuwa umeitendea haki sh500 yako.

Imeandikwa na kuhaririwa na Adson Kagiye
0756508071

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top